UKOSEFU wa mitandao ya maji safi na salama katika
baadhi ya maeneo ya Shinyanga mjini ni miongoni mwa changamoto kubwa
zinazoikabili Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (SHUWASA ) hali ambayo inasababisha baadhi ya maeneo
kukosa huduma muhimu ya maji.
Hayo
yamebainishwa na mkurugenzi mtendaji wa SHUWASA injinia Silvester Mahole wakati
akisoma taarifa kwa mgeni rasmi ambaye alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Annarose Nyamubi kwenye uzinduzi wa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria katika
kijiji cha Ibadakuli katika manispaa ya Shinyanga .
Mahole
alisema mahitaji halisi ya maji kwa wakazi wa Shinyanga mjini ni milimita za ujazo
16,969 lakini wamekuwa wakilazimika kuzalisha maji yenye milimita za ujazo 7000
hadi 8000 kutoka kwenye tenki la maji lililopo eneo la Old Shinyanga
kutokana na kukosekana kwa mitandao ya maji hivyo kufanya matumizi ya maji kuwa
machache.
Alisema
kuwa licha ya SHUWASA kuwa na uwezo wa
kuzalisha maji hayo kwa asilimia 100 kutoka katika vyanzo vyake vya maji kama
vile mradi wa ziwa Victoria pamoja na Bwawa la Ning’hwa lililopo katika wilaya
ya Shinyanga lakini hadi sasa kiwango cha utoaji huduma ya maji safi na salama
kwa wakazi wa mjini Shinyanga ni asilimia 58.5.
“Sababu ya
kutozalisha maji hayo kwa asilimia 100 kwa wakazi wa mjini Shinyanga ni
kutokana na mtandao uliojengwa chini ya mpango wa maendeleo ya sekta ya maji
nchini mjini hapa kwa awamu ya kwanza (Water Sector Development) haukuweza
kufika katika baadhi ya makazi” alisema Mahole.
Akizungumza
katika uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama katika kijiji hicho cha
Ibadakuli Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi ambaye alikuwa mgeni
Rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga alisema mwaka 2007 hadi 2009 mji
huo ulibahatika kupata mradi wa maji lakini kutokana na ufinyu wa bajeti
baadhi ya maeneo miundombinu haikumalizika kujengwa
Nyamubi
alifafanua kuwa kutokana na kutopatikana kwa fedha yote waliyokuwa wameahidiwa
na washirika wa maendeleo (Development Partners) alisema asilimia 50 ya
fedha hizo zilitekelezwa kwa ujenzi wa miundombinu ya maji katika baadhi ya
maeneo huku maeneo mengine yakikosa.
Nyamubi
aliyataja baadhi ya maeneo ya mjini Shinyanga ambayo hajafikiwa na huduma ya
maji safi na salama kutokana na ukosefu wa mitandao ya kusambaziwa maji
kutoka ziwa Victoria eneo la Ngokolo, Mwawaza, Kizumbi,Bugweto,
Chibe,Bushushu pamoja na Kolandoto.
0 Response to "UKOSEFU WA MITANDAO YA MAJI SAFI NA SALAMA HUFANYA BAADHI YA MAENEO KUKOSA MAJI."
Post a Comment