WATU watatu ambao majina yao hawajafahamika wamefariki dunia huku mfugaji
Gilijisiji Gilawida ambaye alichomwa mkuki na kumjeruhi vibaya
sehemu za mwili wake katika
mapigano ya wakulima na wafugaji huko
katika kijiji cha Isakamaliwa kilichopo mpakani mwa mkoa wa Shinyanga na Tabora
ambapo mapigano hayo
yalisababishwa na kugombea mipaka ya malisho.
Hata hivyo kwa upande wa kata ya Magalata wilayani Kishapu mkoani Shinyanga waliopo
wafugaji wengi wa kabila la kitaturu walinyang’anywa mifugo yao zaidi ya 3000 na
wakulima kutoka kijiji hicho kilichopo wilayani Igunga mkoani Tabora huku ikionekana uchochezi huo
kufanywa na wafanyabiashara.
Wakiongea na
mwandishi wa habari katika eneo
hilo baadhi ya wafugaji walisema kuwa chokochoko hizo zimetokana na wakulima kulima
mazao maeneo yote hiyo kusababisha wao kukosa maeneo ya malisho,na wanapo kwenda
kulisha mifugo mara nyingine
huwanyang’anya mifugo yao kwa nguvu jambo ambalo hupingana nalo.
Walisema tayari ng’ombe zaidi ya 3000 wameswagwa na kupelekwa wilaya ya Igunga
jambo ambalo wafugaji hawakukubali hivyo
walianzisha mapigano yaliyosababisha baadhi ya wafugaji kujeruhiwa huku wengine watatu
wakipoteza maisha na mmoja yuko mahututi kwa kujeruhiwa vibaya.
Mmoja wa wafugaji hao
Ndelanha Mahona alisema kuwa mifugo
yake imechukuliwa na wakulima na kuondoka nao wilaya ya Igunga sababu wanayodai
ni mifugo kuingia katika mashamba yao na
kula mazao hali ambayo inaonyesha kuwa ni kuwanyanyasa ikiwa eneo hilo wamekuwa
wakilitumia miaka yote.
Hata hivyo mwenyekiti wa hal mashauri hiyo Justin Sheka alisema kuwa mapigano hayo yametokea hali ambayo
imehatarisha amani kwa wafugaji ikiwa aliwataja walionyang’anywa mifugo hiyo
kuwa ni Ndelanha Mahona,Mbuta Madila Silag’wan
Hendeka, Gidi Babashi, Mfano Gilawida
,Gilajuli Dudula,Magai Dudula,Gishauli Udadi na aliyejeruhiwa ni Gilijisiji
Gilawida.
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya
Kishapu Shija Ntelezu alisikitishwa na
kitendo hicho huku akiitaka serikali
kuthibiti uchungaji holela na kulipatia ufumbuzi suala la mbuga hizo mbili kwani mbuga ya Magalata
ilikuwa ni eneo kwaajili ya malisho lakini wakulima wameliingilia na kufanya shughuli za kilimo holela.
“Serikali lazima ifanye mikakati ya kupata ufumbuzi wa kina
kwenye suala hili kwa watu wameshaanza kuuana hovyo, wadhibiti uchungaji na ukulima holela ikiwa eneo la
Magalata lilitengwa kwaajili ya ufugaji
hivyo liwekewe uzio ,sasa watu
wanafanya shughuli za kilimo bila utaratibu wafugaji wanakosa sehemu za
malisho ndio sababu ya mapigano huku
wafanyabishara wakiwa chanzo chanzo”alisema Ntelezu.
Naye mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku alisema kuwa kweli mapigano hayo yalitokea tangu juzi katika eneo la Magogo linalotenganisha wilaya ya Igunga na Kihspau ikiwa mtu mmoja alifariki dunia wa kutoka wilaya ya Igunga huku wafugaji kutoka Kishapu wakinyang’anywa
mifugo ya zaidi ya 3000 kupelekwa Igunga.
“Tulikaa kamati ya ulinzi na usalama kujadiliana suala hilo
na kwenda katika eneo la mpakani kwenda
kuwasilikiza lakini siku
ilivyofuata ilipata tena taarifa kuwa
mapigano yanaendelea na tayari baadhi ya watu wamejeruhiwa na wengine kuendelea
kupoteza maisha”alisema Nkhambaku.
0 Response to "WATU WATATU WAMEFARIKI DUNIA KATIKA MAPIGANO KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI WILAYA ZA KISHAPU NA IGUNGA"
Post a Comment