Habari za hivi Punde

CHANGAMOTO YA KURIPOTI KWA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA IMEKUWA NI TATIZO MKOANI SHINYANGA.

CHANGAMOTO ya kuozesha wanafunzi wa kike mara wanapohitimu darasa la saba  huku wavulana wakiendelea kutumikishwa na shughuli za uchungaji mifugo na mambo mengine imekuwa  kubwa  ndani ya jamii na kufanya hali  ya kuripoti kwa wanafunzi wa  shule za sekondari waliochaguliwa kuingia kidato cha kwanza  mkoani Shinyanga  kufikia  asilimia 78 .

 Hayo yalisemwa  na mkuu wa mkoa wa huu  Ally Rufunga wakati akiongea na waandishi wa habari  huku akieleza kuwa  wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari wamepata nafasi wote sawa na asilimia 100 lakini kuripoti ndio imekuwa changamoto ambapo watendaji wa vijiji na kata wamepewa jukumu la uangalizi huo ikiwa mwisho wa kuripoti ni mwezi huu.

Alisema  hali ya kuripoti kwa wanafunzi hao ndio imekuwa ni changamoto  baadhi ya wazazi au walezi wamekuwa na tabia ya kutowaruhusu kwa makusudi  watoto wa kike ili waolewe na wakiume kufanya shughuli za kuchunga mifugo   ikiwa kwa  mwaka  wa 2011 mkoa ulifanikiwa  kwa wanafunzi wake kuripoti kwa kiwango cha asilimia 65.8 huku mwaka wa 2012 ilikuwa ni  asilimia 80.3.

 “Changamoto hiyo inatokana na baadhi ya  wazazi kuwaozesha watoto wao pindi wanapomaliza shule ya msingi ikiwa kwa upande wa watoto wa kiume kuangalia mifugo na kutumikishwa shughuli zingine ,ambapo mwisho wa kuripoti wanafunzi hao ni tarehe 28 mwezi huu”alisema Rufunga.

Hata hivyo alisema  kuwa kwa matokeo ya shule za msingi zaidi ya shule  15,000 mkoa wa shinyanga umefanikiwa kuwa katika  nafasi ya 13 ikiwa shule ya msingi  Rocken hill ikishika nafasi ya kwanza  kitaifa kutoka wilayani Kahama ambapo kwa miaka ya 2008 hadi 2010 ilikuwa ikishika nafasi ya mwisho kitaifa.

Hata hivyo  kaimu afisa elimu wa mkoa wa Shinyanga ambaye ni afisa elimu elimu ya watu wazima mkoa huo Yohana Mkumbo alisema  kuwa jumla ya wanafunzi 28,443 ambapo wanafunzi 13604  ndio walifaulu mtihani huo.

Amefafanua kuwa kati ya wanafunzi hao wavulana ni 7460 na wasichana ni 6144 na kuongeza kuwa wilaya ya Kahama inaongoza kwa kufaulisha wanafunzi 3868 ikifiatiwa na wilaya ya halmashauri ya mji wa Kahama iliyofaulisha wanafunzi 2953.

Aidha  mwalimu mkuu wa sekondari ya Bubiki  iliyopo wilayani Kishapu mkoani humo  Mihayo Mashauri  alisema kuwa kupata wanafunzi shule hiyo ni kwaharaka kutokana na kata nzima hakuna shule ya sekondari zaidi ya hiyo huku zikiwepo shule saba za msingi kwenye kata, ambapo shule hiyo ilihitaji wanafunzi  180  kwa mwaka jana lakini walioripoti ni  160 huku sababu ikionyesha wazazi kushindwa kutoa ushirikiano kwa masuala ya elimu dhidi ya watoto wao.

Kwa baadhi ya  wazazi akiwemo Jenipher Luziga  kutoka kata ya  ya Bubiki alisema kuwa tatizo lililopo pia ukosefu wa fedha  ambazo mwanafunzi anatakiwa  iwe kama kianzia kwakwe  mfano wa  fedha za kupata unifomu,michango ya dawati, ada ambapo michango hiyo  inafikia zaidi ya laki moja hivyo mzazi anashindwa kumudu kutokana na kipato  kuwa kidogo  tofauti na  alipokuwa shule ya msingi gharama zilikuwa kidogo.

0 Response to "CHANGAMOTO YA KURIPOTI KWA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA IMEKUWA NI TATIZO MKOANI SHINYANGA."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.