Habari za hivi Punde

MWENYEKITI MPYA WA TIMU YA STEND UNITED ATAKA USHIRIKIANO,ATAJA WACHEZAJI WALIOACHWA KUWA WAKO HURU

MWENYEKITI wa  timu ya Stend United iliyopo mkoani Shinyanga  Ellyson Maeja   ametaka ushirikiano   wa kuinyanyua timu  nakuondoa tofauti zilizokuwepo kipindi cha nyuma   huku akitangaza wachezaji watakao achwa msimu ujao. 

Wachezaji walioachwa na wako huru ni Haruna Chanongo,Nassoro Choro,Rajab Zahir,Hassan Self, Philipo Metusela huku waliomaliza mkataba wao ni  Salum Kamana  na Elius Maturi.


Hayo yalisemwa jana  na mwenyekiti huyo wakati akiongea na waandishi wa habari  siku chache baada ya uchaguzi kufanyika  uchaguzi nakuchaguliwa  huku akisema  kwa mujibu wa katiba  anayo mamlaka ya nafasi za uteuzi ambapo  alimteua Sudi Rashid kwenye  nafasi ya kamati tendaji na Kened  Nyangi  aliamriwa kuendelea na nafasi ya ukatibu kwa muda.
Maeja aliwaeleza waandishi wahabari kuwa lengo lake la baadhi ya wajumbe wa kamati na uongozi  kukutana na waandishi   ni kutaka  mshikamano na  umoja kundeleza soko zuri ndani ya mkoa  ambapo  aliwataka wadau  wasahau yaliyopita.

“Licha ya kumteua Rashid  kwa nafasi hiyo kwa mujibu wa katiba huku moja ikiwa bado wazi ,imeamriwa na kamati tendaji iliyokutana na kukaa kuwa Kenedi  Nyangi aendelee kuwa katibu  wa muda mpaka pale mambo yatakapo kaa sawa  na utaratibu mwingine utafanyika  na katibu msaidizi kamati ilimteua  Emanuel Kaombwe”alisema.

Maeja alisema kuwa Kwa mujibu wa katiba ya shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) na muongozo uliotolewa  mwenyekiti  wa kamati ya  ufundi na usajiri atoke ndani ya  kamati kuu iliyochaguliwa ambapo kamati hiyo  alipendekezwa   mwenyekiti Geofrey Tibakyenda na wajumbe watatu.
Aidha alisema kuwa  tayari timu hiyo  imeongeza  benchi la kocha mwingine wa kigeni  ikiwa kocha mkuu tangu awali alikuwa ni   Patric Liewing, na atakaye kuja kuwa kocha msaidizi  Denis Guillume kutoka nchini uingereza na mtanzania  Athuman Bilal.

Wakati huohuo alisema kuwa  kambi ya  timu ya vijana chini ya miaka 20 itaanza mwezi ujao tarehe mosi  ndiyo maana wameona kuna umuhimu wa kuongeza  nguvu ya makocha ili kupata ushindi

0 Response to "MWENYEKITI MPYA WA TIMU YA STEND UNITED ATAKA USHIRIKIANO,ATAJA WACHEZAJI WALIOACHWA KUWA WAKO HURU"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.