Habari za hivi Punde

MIKAKATI YA KUPINGA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI WILAYANI SHINYANGA

MKUU wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro  ameeleza mikakati dhidi ya kupinga mimba  na ndoa za utotoni  ili kufanikisha   kuwakamata waliosababisha ni wasichana  waliobainika kuwa na mimba kukataa  kusema ukweli  watalazimika  kuwekwa ndani.
Mkuu wa wilaya huyo alisema  hayo  jana alipokuwa mgeni rasmi  mbele ya wadau wa maendeleo katika mradi wa kupinga mimba na ndoa za utotoni kupitia shirika la Agape  ikiwa utekelezaji wake kwenye kata nne za Samuye,Lyabusalu,Iselamagazi

Matiro alisema kuwa katika maazimia ya kikao hicho  uwepo mkakati wa kuwaweka ndani wasichana watakao bainika na mimba kwa kukataa kuwa taja waliohusika  nakuhakikisha hawatoki mpaka pale aliyempa mimba  amefungwa,  kwa kufanya hivyo tatizo la mimba kwa umri mdogo litakaoma.
“Tumekuwa tukipata shida ya kuwabaini watuhumiwa  wanao wapa mimba  ukiachilia wanao fanyiwa vitendo vya ubakwaji ambapo wengi wao huwa katika makubaliano na wazazi kwakuelezwa mtoto  asiseme ukweli ili lengo la wazazi litimie wachukue mahari sasa tatizo hilo tunalikomesha”alisema mkuu wa wilaya.
Hata hivyo alisema kuwa kesi nyingi zimekuwa zikiishia njiani kwa kukosa ushahidi mahakamani na mienendo ya rushwa hivyo  serikali na shirika hili washirikiane kwa pamoja kuteua askari,mwanasheria   maalum watakao simamia masuala ya mimba za utotoni  kwa kuhakikisha mtuhumiwa anakamatwa na kushitakiwa kisha kuhukumiwa hapo tatizo litakoma .
Baadhi ya wadau waliohudhuria kikao hicho  mtendaji wa kata ya Samuye Emanuel  Maduhu  na  Budugu Kasuka  mtendaji  kata ya  Lyabusalu walisema kuwa  msichana atakaye bainika kuwa na mimba pindi akihojiwa na kuleta ubabaishaji  wote watawekwa ndani  kwani  wataangalia na mazingira ya  mtoto mwenyewe  alivyoipata.
“Wazazi wengine  pia wanaona msichana umri mdogo kupata mimba ni dili kwao kuwa watapata faida  hasa akieleza mtoto mimba hiyo ni kutoka  familia yenye uwezo ,mahari  yenyewe inakwenda kuchukuliwa kijiji  au mkoa mwingine kwa kuhofiwa kukamatwa sisi viongozi tutaangalia   kwanza mzazi alichukua hatua gani baada ya kubaini  kama kuna ubabaishaji wote wawekwe ndani”alisema  mtendaji wa kata ya Lyabusalu Kasuka.
Naye  Stanley  Mref  mwenyekiti wa  kamati ya ulinzi   na usalama wa mtoto kutoka  halmashauri ya wilaya ya Shinyanga  alisema kuwa hilo  wazo linaendana na hapa kazi tu basi litekelezwe nakulifanyia kazi katika maeneo yaliyotengwa   ila ushauri ufanyike mkutano wa hadhara  ili kuweza kutoa elimu katika jamii nakuelezwa hayo maazimio.
Mkurugenzi wa shirika  hilo John Myola alisema   mradi uliomalizika katika vijiji kumi ulipunguza tatizo la mimba  ila changamoto bado ipo ya baadhi ya  wazazi kuwapeleka kwa waganga wa kienyeji  wasichana umri mdogo ili wapendwe na wanaume huku kesi nyingi zikiishia hewani kwa kushindwa kutolewa ushahidi

0 Response to "MIKAKATI YA KUPINGA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI WILAYANI SHINYANGA"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.