Maji haya ni mradi kutoka ziwa victoria ,pia wananchi wa vijiji vya Mwakitolyo na Mawemilu halmashauri ya (w) Shinyanga walilia mradi kama huo. |
WANANCHI wa vijiji vya Mwakitolyo na Mawemilu kata ya Mwakitolo halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga wameanza kutekelezewa mradi wa
maji ya ziwa Victoria kutokana na kukabiliwa na keroya uhaba wa maji kwa muda mrefu hali ambayo inawafanya kupata
maji ambayo siyo salama kutoka kwenye chemchem za kuchimba chini nayo
hukauka kwa muda mfupi.
Ahadi hiyo imeanza kutekelezwa kwa kusimamiwa na mbunge wa jimbo hilo Amahed Salum ikiwa tayari tenki la maji limeanza
kukamilishwa lenye ujazo wa lita 90,000 na kufaidisha wakazi zaidi ya 4000
,uliogarimu jumla ya kiasi cha shilingi billion
1.36. ambapo maji hayo yatatengenezewa
mifereji ya kutoa maji ili kuweza kufikia wakazi wa vijiji vyote kwenye kata hiyo.
Baadhi ya wananchi wa
vijiji hivyo kwa nyakati tofauti kilio hicho kwenye mkutano wa hadhara kuhusu changamoto ya
ukosefu wa maji safi na salama kwa
mbunge wao,ambapo wakazi wa kijiji cha Mwakitolyo walilalamika
kuchangishwa kiasi cha shilingi 39,000 kwa kila kaya ili kuweza
kufanikisha mradi huo ikiwa walitaka ufafanuzi
kwanini wanachangishwa kiasi kikubwa
na kwa shughuli gani walihoji.
Mmoja wa wananchi hao
Vicenti Kusekwa alieleza mbele ya mbunge huyo kuwa kero ya maji imekuwa ni tatizo kwa
wananchi,pia mradi huo wameona kuanza kutekelezwa lakini umekuwepo
uchangishwaji wa fedha kila kaya ambazo
hawafahamu zinatumika kufanya nini pia kiwango hicho kinachotamkwa ni
kikubwa hivyo walimtaka mbunge kuondoa
kero hiyo ili waweze kupata maji.
Kwa upande wake mtendaji wa kata hiyo Goodluck Kipilimba alitoa ufafanuzi kuwa waliitisha mkutano wa hadhara na kuwapatia maelezo yote kwa kina namna
sheria inavyotakiwa jinsi ya kuchangia kwenye mradi ikiwa wananchi wanatakiwa
kuchangia robo ya fedha zinazohitajika kwenye mradi huo ikiwa kijiji hiki kina
kaya 942 na ukigawa kwa kiwango kinachotakiwa kila kaya itataikiwa kutoa
shilingi 39,000.
Kaimu mhandisi wa maji Andrew Mogella alielezwa kuwa mradi huo umegharimu
jumla ya shilingi billion 1.3 na kunufaisha wakazi zaidi ya 4000 ikiwa ujanzo wa tanki hilo ni lita 90,000 hivyo tayari ujenzi wa
mifereji ya kupitisha mabomba imewekwa kwa lengo la kusambaza kwenye vijiji
jirani na lililopo tanki hilo.
Mbunge huyo aliwataka kuunda kamati itakayosimamia
fedha za mradi wa maji yenye kuaminika
kwani maeneo mengine wamekuwa hawapeleki
fedha benki wala kuwasomea mapato na matumizi ya fedha hizo na matokeo yake huliwa hovyo, aliwaeleza mradi huu uko mbioni kukamilika wasikubali
kukaa miezi sita bila kusomewa mapato
hayo ni ndani ya mwezi mmoja wasomewe ili kuweza kufamu kiasi cha pesa
kinachopatikana.
“Mradi huo kuja niliupigia
kelele kutoka wizarani, ni mradi mkubwa kati ya miradi mitatu ndani
ya jimbo la Solwa ukianzia wa umeme vijijini,ujenzi wa hospitali ya wilaya na huu wa mwakitolyo kila mmoja umegharimu kiasi cha fedha
kisichopungua billion moja,hivyo mradi wa maji inatakiwa muwe
makini nao na fedha zitakazo patika ni kwaajili ya matengenezo pindi pampu au
pomba kukaribik”alisema mbunge Ahamed.
Alisema kuhusu uchangishwaji wa fedha hizo kiko sahihi kwani
maeneo mengi yenye mradi yamechangishwa
ila kijiji hiki cha Mwakitolyo mnakiona kiwango hicho ni kikubwa
kutokana na idadi ya kaya kuwa ndogo isitoshe haihusishi vijiji vingine ambvyo
viko mbali na tanki,ikiwa sheria iliyopo
halmashauri katika mradi huu itachangia kiasi cha shilingi million 36 na kingine wananchi wemyewe na
asilimi 75 hutolewa na benki ya dunia ambao
ni wafadhili.
.
0 Response to "WANANCHI WA VIJIJI VYA MWAKITOLYO NA MAWEMILU WALILIA MRADI WA MAJI WA ZIWA VICTORIA."
Post a Comment