Habari za hivi Punde

WATU WAWILI WAMEFARIKI KATIKA MACHIMBO YA DHAHABU KWA KUKOSA HEWA

WATU wawili wamefariki dunia ambao ni  Lingwa Buluguti (35) na  Simba  Mayeka (55) wote wakazi wa kijiji cha Mwakitolyo wilayani Shinyanga  walifariki mara baada ya kukosa hewa katika shimo walilokuwa wakichimba mchanga udhaniwao na dhahabu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Justus  Kamugisha aliwaeleza waandishi wa habari kuwa  marehemu hao  walifariki mnamo majira ya saa tisa  alasiri wakati wakichimba mchanga ndani ya shimo muda mfupi udongo uliwafunika na kisha kukosa hewa.

KARENY. Powered by Blogger.