Kijana akiwa amebeba madumu ya maji tayari kwa biashara.
WANANCHI wa Halmshauri ya Mji wa bariadi Mkoani simiyu, wameiataka serikali
mkoani hapa kuwatatulia kero ya maji iliyopo kwa sasa, kutokana na kutumia muda
mwingi kutafuta maji ikiwa katika kero
hiyo vijana wameweza kujipatia kipato kwa kuuza dumu moja shilingi 500 tipu
moja ya tolori lenye madumu sita shilingi 4000 hadi 5000.
Wananchi hao wamebainisha kuwa vituo vya kupatia maji vilivyoko chini ya
mamlaka ya maji katika mji wa bariadi, ndani ya wiki 2 vimekuwa havitoi maji na
kuwalazimu kutumia muda mwingi kufuata hudua hiyo katika visima vya watu
binafsi.
Wakiongea na waandishi wa habari
katika visima mbalimbali vya maji vya watu binafsi vilivyoko mjini hapa,
wananchi hao wamesema kuwa wamekuwa wakiangaika kupata maji huku vituo
vinavyomilikiwa na mamlaka ya maji mjini hapa kutoa maji mara moja kwa wiki.
Hata hivyo vijana katika mji huo
wamejipataia ajira kutokana na kuwepo kwa uhaba wa maji kwa kiasi kikubwa,
ambapo dumu moja la maji linauzwa kwa shilingi 500 huku tiripu ya torori lenye
dumu 6 likiuzwa kwa shilingi 4000 hadi 5000.
Akiongelea juu ya kero hiyo
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji ya mji wa Bariadi Richard Magwizi alisema kuwa
chanzo cha kukosekana kwa maji katika vituo ni kuwepo kwa ukarabati wa mashine
ya kusukuma maji katika moja ya kisima kikubwa kilichopo mjini hapa katika kata
ya sima kijiji cha Mahaha.
|
0 Response to "VIJANA WAONGEZA KIPATO KUPITIA SHIDA YA MAJI MJI WA BARIADI"
Post a Comment