HIKI NI CHOO KINACHOTUMIWA NA WANAFUNZI ZAIDI YA 500 SHULE YA MSINGI MAWEMILU.
SHULE ya msingi
Mawemilu iliyopo katika kijiji hicho kata ya Mwakitolyo halmashauri ya Shinyanga inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa matundu ya vyoo vya wanafunzi pamoja na walimu hali
ambayo inawafanya kuwepo kwa uchafuzi wa
mazingira kwa kujisaidia porini huku walimu wakitumia vyoo vya familiza za walimu zilizopo karibu
na shule hiyo.
Shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi zaidi ya 500 ikiwa
wavulana 211 na wasichana 300
ambapo choo kilichopo kina matundu
mawili pekee hata miundombinu yake ni
mibovu iliyojengelewa kwa nyasi huku walimu wakiwa 11 wakiume saba na wakike
wanne,sanjari na robo tatu ya shule hukalia magogo ya miti wawapo darasani.
Mwandishi wa habari mara baada ya kujionea changamoto hiyo
alifanikiwa kuonana na Mwalimu mkuu wa shule hiyo Joseph Chagaka ambaye alikiri kuwepo kwa changamoto hizo huku akisema kuwa awali kulikuwepo na matundu ya vyoo sita kwa wanafunzi lakini
yalititia kutokana na mvua za masika
zilizokuwa zikinyesha,kwa upande wa vyoo vya walimu havikuwepo.
“Kweli changamoto hiyo
ipo sisi tuliamua kujenga choo hicho chenye matundu mawili na kujengelea
kwa nyasi wanafunzi watumie kwa muda tukiwa tunaendelea kujipanga na
ujenzi,nina amini havitoshelezi kwani kuna wanafunzi zaidi ya 500, madawati
yapo 50 tu, walimu wapo 11 nyumba za walimu zipo mbili ila choo cha walimu shuleni hapa hakuna
hutumia vyoo vya kwenye familia za walimu.”alisema mwalimu mkuu huyo.
Hata hivyo mwalimu mkuu huyo alisema kuwa kuna mahitaji makubwa ya
madawati,matundu ya vyoo kumi na moja, vyumba vya madarasa ,walimu 21 na
nyumba za walimu 11 ili kuweza kutosheleza,ila mikakati iliyopo ni kuzipunguza
changamoto hizo zimekuwa ni kero hali ambayo imeonekana hata wanafunzi na
walimu wenyewe kupata usumbufu .
Naye ofisa mtendaji
wa kijiji hicho Ezekiel Deusi alisema kuwa changamoto kubwa shuleni hapo ni vyoo vilivyopo miundombinu yake ni mibovu ni sawa
na hakuna vyoo kwani vilititia kipindi cha mvua
za masika na sasa mahitaji ni
matundu ya vyoo 11 ili kuweza
kuondoa changamoto hiyo, mikakati ya ujenzi inafanyika ikiwemo vyoo vya walimu pia, ambapo suala la madawati wanafunzi
robo tatu ya shule hukalia magogo
ya miti wakiwa darasani yanahitajika
madawati kwa wanafunzi hao.
Ofisa elimu msingi Andrew
Mitumba wa halmashauri hiyo alisema kuwa kero hiyo ni muda mrefu kwani
mwalimu mkuu alikwisha andikiwa barua
ya onyo kwa uzembe kwa kutotekeleza changamoto za ukosefu wa vyoo kwa wanafunzi haraka
kwani wazo la kuwa na shule linatoka
kwenye serikali ya kijiji na wizara
inaridhia kwa kuangalia vigezo vyote kama vimetizmizwa ikiwemo vyoo, huu ni
uzembe wa wananchi pamoja na viongozi wa
serikali ya kijiji.
“ Isitoshe kuna fedha za ruzuku hutolewa kwa shule za msingi
ambazo anatakiwa achukue kidogo na
kuanzisha ujenzi ikiwemo na michango kwa wananchi ili halmashauri iweze kukamilisha lakini huyu mwalimu mkuu hafanyi hivyo kama
alivyoelekezwa,pia suala la ukosefu wa
madawati shuleni hapo lipo kwani
halmashauri imetenga fedha kwaajili ya kupata madawati 513 na mipango ni kuzigawia shule ambazo hazina
madawati sanjari na shule ya msingi hii
.
.
|
0 Response to "SHULE INAKABILIWA NA UKOSEFU WA CHOO CHA WANAFUNZI ZAIDI YA 500,PAMOJA NA WALIMU IKIWEMO MADAWATI."
Post a Comment