BAADHI ya wananchi wa kijiji cha Igalamya kata ya Usule
katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wamelalamika kutozwa gharama ya shilingi
40,000 hadi 60,000 ya usafiri wa gari la
wagonjwa (Abulance)pindi wanapokuwa na wagonjwa wanaohitajika kwenda
kupata matibabu zaidi kwenye hopitali ya
rufaa ya mkoa
Hali hiyo imewafanya baadhi ya wagonjwa kupoteza maisha wakiwa njiani huku mama wajawazito kuzalia majumbani au njiani kwa kukosa gharama hiyo
ambayo ilikuwa ikitozwa na waganga wa
vituo vya afya kwa kudai ni gharama za mafuta ya kumpeleka mgonjwa
hospitali ya rufaa ambayo iko mjini.
Wananchi hao wakiongea kwenye mkutano wa hadhara mbele ya mbunge wa jimbo hilo la Solwa Ahamed Salum uliofanyika katika kijiji
hicho, mara baada ya kukabidhiwa gari hilo baada ya kuharibika kwa
muda mrefu bila kupatikana mtu wa kulitengenezai ndipo aliamua mbunge kulitengeneza kwa gharama yake ya shilingi millioni 7.5.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo akiwemo Mariamu Malale
na Elius Bukwiba walisema
kuwa walikuwa wakitozwa kiasi cha
shilingi 40,000 hadi 60,000 na uongozi
wa zahanati hiyo kwa kukodi gari
la wagonjwa kumpeleka mgonjwa katika
hopitali ya rufaa mjini hata ukiwa na mama mjazito wengi walikuwa wakitoa ambao
hawana mara nyingi wagonjwa walikuwa wakizidiwa njiani na kupoteza maisha.
“Mimi mwenyewe nimekwisha toa kiasi cha shilingi 40,000 kwaajili ya gari kumpeleka mtoto wangu
hospitali ya rufaa mjini ili kuweza
kupata matibabu,nilipokuwa natoa pesa hizo nilielezwa kuwa ni gharama za mafuta
kwasababu nilikuwa nataka mtoto wangu apone nilitoa sikufahamu kuwa ni bure
kama inavyoelezwa sasa na mbunge kweli tumeteseka na huo ndio utakuwa ni mkombozi wetu”alisema Bukwiba.
Naye mbunge wa jimbo
hilo Salum alisema kuwa gari hilo amelileta kwa matumizi ya rufaa pekee ambapo watakuwa
wakisafirishwa bure atakaye toa pesa awe
amependa mwenyewe, mafuta yatakuwepo kila wakati, ila wagonjwa watakao hitajika
zaidi ni mama wajawazito walioshindwa
kujifungua, waliopata ajali na wagonjwa mahututi.
“Nataka niwaeleze kuwa
leo nimekuja kukabidhi gari lililowashinda kulitengeneza sasa nimetengeneza kwa gaharama yangu ya
shilingi millioni 7.5, litabeba wagonjwa waliomahututi bure mafuta yatakuwepo kila wakati ila ninachowaomba hii zahanati
malengo yake ilitakiwa kiwe kituo cha afya kwani nilikwisha leta mifuko
ya saruji 262 haijulikani imekwenda wapi nitaomba kamati iliyoundwa ya usimamizi wa
ujenzi huo inipatie maelezo”alisema
Mbunge Salumu.
Pia mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mohamed
Kiyungi alisema kuwa huduma ya
gari la wagonjwa ni bure hakuna wakuwatoza fedha ya aina yoyote huku akiwahakikishia upatikanaji wa mafuta
kwenye gari hilo utakuwepo hivyo wananchi wasiwe na hofu juu ya hilo kinachotakiwa ni utaratibu wa
utumiaji wa gari la wagonjwa sio kiholela.
Aidha alisema kuwa
wananchi wajitahidi katika mchango ili kuweza kufanikisha ujenzi wa kituo cha afya ikiwa mbunge tayari kajitolewa
mifuko ya saruji hivyo waweke umoja wa kujitolea hata ubebaji
wa michanga na kokoto kwenye ujenzi huo
ili iweze kufanya kazi mara moja na kupunguza
matatizo ya kusafiri umbali mrefu.
|
0 Response to "USAFIRI HUU NI BURE KWA WAGONJWA WENYE KUHITAJI RUFAA,ASEMA MBUNGE."
Post a Comment