HILI NI BARAZA LA MADIWANI MUHEZA.
BARAZA la madiwani wa halmashauri ya
wilaya ya Muheza mkoani Tanga wamemchangua Rashidi Mdachi ambaye ni diwani wa
kata ya Pongwe kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo.
Katika uchaguzi huo uliofanyika juzi
kwenye mkutano wa baraza la madiwani lililo la kawaida,Mdachi ameshinda kiti
hicho baada ya kuchaguliwa kwa kupata kura 37 kati ya 40 zilizopigwa ambapo
kura tatu zilimkataa.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya
Muheza,Amiri Kiroboto akimtangaza,Mdachi juu ya kushinda kiti hicho huku
alisema kura zilizopigwa ni za ndiyo na hapana baada ya mjumbe huyo kupitishwa
katika uchaguzi wa ndani wa CCM huku baraza likikosa wajumbe kutoka upinzani.
"Ndugu wajumbe sasa natakata
kutangaza matokeo baada ya kufanikisha zoezi letu la kupiga kura,awali
tulikubaliana kuwa kura zitakazopigwa ni zile za ndiyo na hapana ambapo sasa
natangaza matokeo,Mdachi amepata kura 37 kati ya 40 na tatuz zimesema hapana"alisema.
Akitoa shukrani mara baada ya kutangazwa
kuwa msindi Mdachi aliahidi kuendelea kutekeleza wajibu wake kwa ufanisi kama
alivyokuwa akiwajibika awali katika nafasi hiyo ambapo pia aliwaomba wajumbe
wenzake kuendelea kumpatia ushirikiano wa hali na mali.
Alisema kuwa ni lazima ieleweke kwamba
hata yeye ni binadamu hivyo anahitaji kuelezwa pale anapokwenda tofauti ambapo
itaweza kuwa vigumu kama hatakumbushwa ama kuelezwa juu ya pale ambapo
amekwenda tofauti ili kuweza kujirekebisha ili kuweza kuwajibika kikamilifu.
Mdachi aliendelea kusema kwamba kitu
kikubwa kinachohitajika kwa sasa ni juu ya kuongezeka kwa mshikamano miongoni
mwa wajumbe na hata watendaji wa halmashauri njia ambayo itawawezesa
kuwatumikia vyema wakazi wa halmashauri ya Muheza na vitongoji vyake.
Aidha makamu mwenyekiti huyo wa
halmashauri ya wilaya ya Muheza alisisitiza kwamba atahakikisha kwamba utoro wa
wanafunzi shuleni unadhibitiwa kwa kushirikiana na wadau wengine ambapo kwa
kufanya hivyo sekta ya elimu itaweza kuimarika na kuleta tija.
|
0 Response to "DIWANI WA KATA YA PONGWE MUHEZA AMECHAGULIWA KUWA MAKAMU MWENYEKITI."
Post a Comment