Habari za hivi Punde

SHULE YA SEKONDARI CHENGE HUKATISHA MASOMO KWA KUKABILIWA NA UHABA WA MAJI.

 KAIMU MWALIMU MKUU  STEVE  MASINDE WA SHULE YA SEKONDARI  CHENGE ILIYOKO BARIADI AKIONYESHA SHIMO KWA WAANDISHI WA HABARI AMBAO HAWAPO PICHANI NAMNA WALIVYOCHIMBA KUTAFUTA MAJI.

Walimu Shule ya sekondari Chenge iliyopo katika Halmshauri Mji wa Bariadi mkoani Simiyu wanakabiliwa na na changamoto mkubwa ya uhaba wa maji hali inayowafanya wao pamoja na wanafunzi kushindwa kuhimili hali hiyo na kuamua kuondoka shuleni hapo kila siku kabla ya muda.
 
Walisema hali hiyo imeongeza utoro kwa wanafunzi na wakati mwingine kusababisha baadhi ya masomo kutofundishwa kutokana na wanafunzi kutumia muda huo, kufuata maji umbali wa kilometa moja katika mto wa nyaumata ambao walisema nao umekauka.
 
Akiongea na wandishi wa habari shuleni hapo kaimu mkuu wa shule hiyo Steven Masinde alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa shule hiyo kwa muda wa miaka 7 wamekuwa wakiangaikia kero hiyo kuipeleka katika ngazi za juu za serikali lakini bila ya mafanikio.
 
Masinde alibainisha kuwa mwaka 2010 wananchi wa kijiji walichimba kisima shuleni hapo, na kuishia katikati bila ya kumalizika. Huku diwani wa kata Robert Rweyo naye akichimba shimo ambalo nalo lilishia njiani bila ya kumalizika.
 
“kwa sasa shule imejaa mashimo..ambayo ni hatari kwa wanafunzi hata familia za walimu wanaoishi katiba nyumba za shule..kuna shimo la wananchi halikumalizika, lakini diwani naye alichimba akakomea njiani..yote yapo hayana kazi na sasa yameanza kutupiwa uchafu na wanafunzi” Alisema Masunga.
 
Alisema kuwa walimu wengi wanaoletwa shuleni hapo wamekuwa wakikataa kuishi karibu na shule hiyo kutokana na kukosa maji hata ya kunawa mara baada ya kutoka darasani kwa ajili ya kutioa uchafu wa chaki, huku wanafunzi wakikosa hata maji ya kunywa.
 
Aidha alisema kuwa walimu wengi wamekuwa wakiishi mjini Bariadi ambapo ni urefu wa kilometa 10 kutoka shuleni hadi mjini, jambo linalosababisha walimu hao kuondoka shuleni hapo kabla ya muda wa kazi.
 
Hata hivyo Masinde alisema wameanziasha mpango wa chakula kwa wanafunzi hususani madarasa yenye mitihani, kidato cha pili na nne lakini wanashindwa kumudu kwa sababu ya kukosa maji na kuwalazimu wanafunzi waache vipindi na kwenda kutafuta maji katika mto nyaumata.
 
Alibanisha maji ya mto huyo yamekuwa siyo salama na kutishia uhai wa maisha yao, kutokana mto huo kukauka hali inayowalazimu kuchimba mashimo kwa ajili ya kupata maji, huku wakichangia mto huo pamoja na mifugo.
 
Hata hivyo shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 232 ilianzishwa mwaka 2007 inakabiliwa na uhaba wa walimu wa sayansi hadi sasa ina mwalimu mmoja wa sayansi ikiwa pamoja na ukosefu wa nyumba za walimu na thamani za ofisi.

KARENY. Powered by Blogger.