Habari za hivi Punde

CHANZO CHA KUKITHIRI KWA MAUAJI YA VIKONGWE CHABAINISHWA

MKUU wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya.


  
  KUSHAMIRI  kwa matukio hayo ya mauaji kwa kukatwa mapanga kwa akina mama katika mkoa wa  Shinyanga kwa asilimia kubwa kunasababishwa na viongozi wa serikali za vijiji ambao hukosa uzalendo kutokana na  kugeuza matukio hayo kuwa vyanzo vya mapato yao kwa kuwahifadhi watuhumiwa wa vifo hivyo ambavyo hudaiwa husababishwa na imani za kishirikina..
Mkuu huyo wa wilaya, aliwashutumu viongozi wa  serikali za vijiji kwa kutokuwa waadirifu na kusahau miiko yao ya uongozi kwa kuwakumbatia wauaji wa akina mama ambao wengi huuawa kuanzia miaka 45 huku wakitambua fika tabia hizo zinakwamisha jitihada za serikali za kuwatia mbaroni na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika hao.
Alisema mauaji hayo huwa vitega uchumi wa viongozi wa serikali za vijiji wa eneo lililotokea tukio ambapo hushindwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi badala yake huchukua fedha kwa wauaji ili wawahifadhi hivyo kufanya vita dhidi ya mauaji ya   kuwakata mapanga akina mama kwa  imani za kishirikina,kuendelea kuwa janga kubwa pamoja na viongozi mbalimbali wa dini na serikali kupigia kelele ya hali hiyo.
.
Mpesya alisema upo ushahidi wa kutosha kwa baadhi ya matukio ya mauaji ya vikongwe yanapo tokea ,mara nyingi wenyeviti wa vijiji hubaininka  kuwaficha watuhumiwa wa mauaji, na tayari mwenyekiti mmoja ameshikiliwa  (hakumtaja jina) baada ya kub ainika kupokea shilingi million tatu (3,000,000) kutoka kwa watuhumiwa wa mauaji ili awahifadhi.
Aidha kuhusu  kukwama kwa kesi hizo mahakamani pindi watuhumiwa wanapofikishwa mbele ya sheria kunatokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani watuhumiwa wa mauaji hayo baada ya mashahidi kuepuka kutoa ushahidi kwa hofu nao kukumbwa na mauti kutoka kwa  baadhi ya wauaji hao ambao wanakuwa  hawajakamatwa.
Pia alisema wapo wasamalia wengine hujitolea kutoa ushahidi lakini wengi wao wamekimbia familia zao au kuhama kabisa maeneo yao kwa vitisho mbalimbali ambavyo hutolewa na baadhi ya wauaji, hali ambayo pia imechangia kwa watu wanao wafahamu wauaji hao kushindwa kujitokeza hadharani kutoa ushahidi
Hata hivyo serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kutoa elimu juu ya umuhimu wa ushahidi katika kesi za mauaji hayo ambayo pamoja na kuwa ya hatari lakini wauaji wanajulikana ni kikosi cha kukodi kati ya shilingi laki tatu hadi tano kwa kuua mtu mmoja .
Wilaya ya Kahama ni miongoni mwa maeneo ya kanda ya ziwa yanayo ongoza kwa wazee wenye macho mekundu kuuawa kwa kukatwa mapanga huku watuhumiwa wengi wao wakikamatwa na polisi na baadae kuachiwa na Mahakama baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kuwatia hatiani kunakosababishwa na jamii kukosa ujasiri wa kwenda mahakamani
Kamugisha alifafanua katika kipindi cha Mwezi Januari hadi Decemba mwaka jana (2013), katika halmashauli ya wilaya ya Shinyanga Vijijini wameuawa Vikongwe 11, Kahama 9,  Kishapu 7, ikiwa jumla ya vikongwe 27 waliouawa katika kipindi hicho.

Aliendelea kufafanua katika kipindi cha Mwezi januari hadi julai mwaka huu (2014), wameuawa vikongwe 11,halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini 6,  Kahama 4, Kishapu Mmoja, huku jumla kuu ya vikongwe waliouawa katika kipindi cha mwaka Jana hadi julai (2014 ), ni Vikongwe 38.

0 Response to "CHANZO CHA KUKITHIRI KWA MAUAJI YA VIKONGWE CHABAINISHWA"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.