CHANGAMOTO ya kuozesha wanafunzi wa kike mara wanapohitimu
darasa la saba huku wavulana wakiendelea
kutumikishwa na shughuli za uchungaji mifugo na mambo mengine imekuwa kubwa ndani ya jamii na kufanya hali ya kuripoti kwa wanafunzi wa shule za sekondari waliochaguliwa kuingia
kidato cha kwanza mkoani Shinyanga kufikia asilimia 78 .
Hayo yalisemwa na mkuu wa mkoa wa huu Ally Rufunga wakati akiongea na waandishi wa
habari huku akieleza kuwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya
sekondari wamepata nafasi wote sawa na asilimia 100 lakini kuripoti ndio
imekuwa changamoto ambapo watendaji wa vijiji na kata wamepewa jukumu la
uangalizi huo ikiwa mwisho wa kuripoti ni mwezi huu.
Alisema hali ya
kuripoti kwa wanafunzi hao ndio imekuwa ni changamoto baadhi ya wazazi au walezi wamekuwa na tabia
ya kutowaruhusu kwa makusudi watoto wa
kike ili waolewe na wakiume kufanya shughuli za kuchunga mifugo ikiwa kwa
mwaka wa 2011 mkoa
ulifanikiwa kwa wanafunzi wake kuripoti
kwa kiwango cha asilimia 65.8 huku mwaka wa 2012 ilikuwa ni asilimia 80.3.
“Changamoto hiyo
inatokana na baadhi ya wazazi kuwaozesha
watoto wao pindi wanapomaliza shule ya msingi ikiwa kwa upande wa watoto wa
kiume kuangalia mifugo na kutumikishwa shughuli zingine ,ambapo mwisho wa
kuripoti wanafunzi hao ni tarehe 28 mwezi huu”alisema Rufunga.
Hata hivyo alisema kuwa kwa matokeo ya shule za msingi zaidi ya
shule 15,000 mkoa wa shinyanga
umefanikiwa kuwa katika nafasi ya 13
ikiwa shule ya msingi Rocken hill ikishika
nafasi ya kwanza kitaifa kutoka wilayani
Kahama ambapo kwa miaka ya 2008 hadi 2010 ilikuwa ikishika nafasi ya mwisho
kitaifa.
Hata hivyo kaimu
afisa elimu wa mkoa wa Shinyanga ambaye ni afisa elimu elimu ya watu wazima
mkoa huo Yohana Mkumbo alisema kuwa
jumla ya wanafunzi 28,443 ambapo wanafunzi 13604 ndio walifaulu mtihani huo.
Amefafanua kuwa kati ya wanafunzi hao wavulana ni 7460 na
wasichana ni 6144 na kuongeza kuwa wilaya ya Kahama inaongoza kwa kufaulisha
wanafunzi 3868 ikifiatiwa na wilaya ya halmashauri ya mji wa Kahama
iliyofaulisha wanafunzi 2953.
Aidha mwalimu mkuu wa
sekondari ya Bubiki iliyopo wilayani Kishapu mkoani humo Mihayo Mashauri alisema kuwa kupata wanafunzi shule hiyo ni
kwaharaka kutokana na kata nzima hakuna shule ya sekondari zaidi ya hiyo huku
zikiwepo shule saba za msingi kwenye kata, ambapo shule hiyo ilihitaji
wanafunzi 180 kwa mwaka jana lakini walioripoti ni 160 huku sababu ikionyesha wazazi kushindwa kutoa ushirikiano kwa masuala ya elimu dhidi ya watoto wao.
Kwa
baadhi ya wazazi akiwemo Jenipher Luziga kutoka kata ya ya Bubiki
alisema kuwa tatizo lililopo pia ukosefu wa fedha ambazo mwanafunzi
anatakiwa iwe kama kianzia kwakwe mfano wa fedha za kupata
unifomu,michango ya dawati, ada
ambapo michango hiyo inafikia zaidi ya laki moja hivyo mzazi
anashindwa kumudu kutokana na kipato kuwa kidogo tofauti na alipokuwa
shule ya msingi gharama zilikuwa kidogo.
0 Response to "CHANGAMOTO YA KURIPOTI KWA WANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA IMEKUWA NI TATIZO MKOANI SHINYANGA."
Post a Comment