SHULE ya sekondari
Masekelo iliyopo kwenye kata hiyo manispaa ya Shinyanga inakabiliwa na changamoto mbalimbali ya kukosa eneo kwaajili viwanja vya michezo,
mashamba ya kulima vyakula ,uhaba wa maji , hali ambayo inawafanya wanafunzi wa shule hiyo kukosa haki zao za
msingi.
Zoezi la utekelezaji kilimo cha mtama kwa shule hiyo halipo
sababu ya kukosa mashamba,hakuna eneo lililotengwa viwanja vya michezo ikiwa wananchi wanalima
mpaka nyuma ya madarasa ya shule huku
bado wenye mashamba yao walionyang’anywa na manispaa hawajalipwa fidia,pia
haina maji ingawa wanapata uji wanafunzi shuleni hapo kwa kulipia shilingi 40,000 kwa mwaka.
Mkuu wa shule
hiyo Stephen Mihambo aliongea na baadhi ya waandishi wa habari waliotembelea shuleni
hapo huku akieleza kuwa shule inajumla ya wanafunzi 319 ,vipindi vya michezo vipo ila hakuna
uwanja wa michezo, hali inayojionyesha ni mwamko mdogo wa jamii katika suala
zima la elimu kwa kushindwa kutoa maeneo
ya mashamba yao ili shule ipate viwanja vya michezo.
“Katika suala la maji lilifanyiwa makadirio mwaka 2012 kwa kuishirikisha mamlaka ya maji safi na
mazingira (Shuwasa), ili yapatikane
maji ya bomba kwakuhitajika zaidi ya
shilingi millioni 28, ila kwa sasa
linafanyiwa mchakato na kuahidiwa
katika fedha za mfuko wa jimbo suala
hilo litatekelezwa ila kwa sasa maji yanayopatikana shuleni hapo huwapatia tenda watu na kutofahamu yanatolewa wapi salama au si
salama”.alisema Mihambo.
Ambapo
alisema kilimo cha mtama shuleni hapo kutokana na kampeni inayofanywa
na serikali ya mkoa kuwa kila shule ilime angalau ekari mbili za mtama
kimeshindikana ili kupatikane chakula , sababu ya kukosa mashamba ya
kulima ili kuweza kupunguza tatizo la uchangishwaji fedha kwa wazazi
kwaajili ya uji au chakula cha mchana.
Kaimu afisa mtendaji wa kata hiyo Ester Daudi alisema kuwa suala zima la changamoto hizo kweli ila kwa
upande wa mashamba wananchi bado hawajalipwa
fidia ambapo liliwasilishwa manispaa,suala la uhaba wa
maji kwa kukosa mabomba lipo na lilijadiliwa mara baada ya kupokea barua ya uthibitisho wa
fedha za jimbo tayari kumependekezwa
kutekeleza upatikanaji wa maji ya bomba shuleni hapo.
Naye diwani wa kata hiyo Zacharia Mfuko alikiri kuwepo kwa
changamoto hizo shuleni hapo huku akisema kuwa
tangu mwaka wa 2012 suala hilo limeanza kuzungumziwa katika manispaa na mchakato bado unaendelea
ila maji yanayopatikana kwa sasa katika shule hutoka sehemu mbalimbali nje ya
kata hiyo hali ambayo inaonyesha hata kuhatarisha afya za watumiaji.
Alisema kuwa mashamba hayo wananchi bado hawajalipwa fidia tangu mwaka 2007,ikiwa
suala hilo mpaka sasa lipo kwenye ofisi ya mipango miji
na linafanyiwa kazi pamoja na hayo shule
kweli inatatizo la ukosefu wa uwanja wa michezo
naye mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Deogratius Shitenge alikiri kuwepo kwa
changamoto hizo huku akieleza kuwa vikao vimekaa na kuahidi kuyatekeleza ikiwa
fedha zitapatikana.
Baadhi ya wananchi wa kata hiyo akiwemo Monica Ndalu na Kwilasa
Mahene walisema kuwa maeneo yao
yalichukuliwa kwa lengo la kupisha ujenzi wa shule lakini mpaka sasa bado hawajalipwa fidia ambapo sehemu ya mashamba
yaliyokaribu na shule hiyo wanalazimika kuyaendeleza kwa kukosa maeneo mbadala kwaajili ya kilimo
.
0 Response to "SHULE YA SEKONDARI MASEKELO INAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI IKIWEMO UKOSEFU WA VIWANJA VYA MICHEZO,UHABA WA MAJI PAMOJA NA MASHAMBA"
Post a Comment