Habari za hivi Punde

SHULE ZA MSINGI TATU KATA YA NDEMBEZI MANISPAA YA SHINYANGA ZAPATA MSAADA WA MAHINDI
SHULE za msingi  tatu zilizopo  kata ya ndembezi  manispaa ya shinyanga  zimepatiwa jumla ya magunia  kumi na moja ya  msaada wa mahindi yenye thamani ya shilingi  lakitano na nusu kwaajili ya  wanafunzi kupata  uji asubuhi  wakiwa shuleni hapo ili kuondokana na ubagudhi wa wasiolipa fedha kutokunywa uji na waliolipa kunywa.
Msaada huo wa mahindi yaliyotoka kwenye kitengo cha maafa ofisi ya waziri mkuu na kuamua kuyanunua    diwani wa kata hiyo David Nkulila  ambaye pia ni naibu meya wa halmashauri  ya manispaa hiyo  kwa gunia moja shilingi 500 huku akidai kuwa  aliamua kutoa msaada  kutokana na  baadhi ya wazazi kushindwa kutoa mchango wa kupata uji wanafunzi .


Nkulila akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutoa msaada huo  alisema kuwa  hali halisi ya  wanafunzi  kupata uji asubuhi aliiona,  ambapo imeonyesha  kuwa waliolipa  fedha  wanakunywa na ambao hawajalipa hawanywi hilo ni tatizo ambalo linaweza kujenga matabaka hapo badaye.

 Zoezi la unywaji uji na ambao hawanywi nimeliona ikiwa linaweza pia   kumharibu  kisaikolojia  mtoto kwa kujisikia vibaya akiwa hanywi uji huku wengine wakinywa huku akiwaangalia  wenzake hiyo nayo imekuwa changamoto nawaomba wazazi kuendelea kujitoa kwa michango ili kuondoa tabaka hilo linalojitokeza ila kweli mimi roho inaniuma kwa kuona hali kama hii inakuwepo mashuleni”alisema Nkulila.


Hata hivyo alizitaja shule hizo kuwa ni Bugaoyi A  imepata gunia tatu,Bugoyi B gunia tatu ,  isipokuwa shule ya msingi Ndembezi  imepata gunia tano ambazo zitawasaidia watoto wote kunywa uji bila kuangalia aliyechanga na asiyechana.

 kwa upande wake afisa elimu kata  ya ndembezi  Selemani Bulugu alisema kuwa  mahindi hayo yametolewa katika shule hizo kwa msaada wa diwani huku akiyagharimia gunia moja shilingi 5000  ambapo wazazi wataendelea kuchangia huduma zingine muhimu zinazohitajika ili wanafunzi waweze kunywa uji huo.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya  Msingi Bugoi A Anord Rushabura  alisema kuwa utaratibu uliokuwepo  wazazi wanatakiwa kuchangia shilingi 4000 kwa mwezi  au shilingi 200 kwa siku ikiwa shule hiyo inawanafunzi zaidi ya  900  ambapo mchango huo  ulilenga kufanikisha  mahitaji muhimu kama sukari na unga ikiwa mzazi hata toa fedha hiyo hatapata huduma ya kunywa uji mtoto wake  shuleni hapo.

Baadhi ya wazazi  wanaosomesha watoto wao katika shule ya msingi Bugoyi A  Leokadia Ndyalu na Doto Jilinde  walisema gharama za shule zinaongezeka  huku wakiitaka serikali kusaidia suala la chakula mashuleni  ambapo  walidai kuelemewa na msongamano wa michango mbalimbali ikiwemo madawati,na fedha kwaajili ya mlinzi na maji.
.
KARENY. Powered by Blogger.