Habari za hivi Punde

WANAFUNZI KUSHINDA BILA KUNYWA MAJI,SHULE YAAMUA KUCHIMBA KISIMA

kijana akichimba shimo kwa lengo la kutafuta maji kwaajili ya wanafunzi wa shule ya msingi Kano iliyopo kijiji cha Amani  kata ya Salawe  halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mara baada ya wanafunzi kukumbwa na kero ya ukosefu wa maji ya kunywa shuleni hapo na kuwafanya washinde bila kunywa maji mchana kutwa ambapo wazazi na walezi waliamua kuchanga pesa lengo kuchimbwe kisima kirefu kitakachotoa maji kwaajili ya wanafunzi wa shule hiyo .

Aliyevaa koti ni mwenyekiti wa kijiji cha Amani  Dotto Polepole  akiwa na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kano Shabani  Masuma  wakielezea changamoto kubwa shuleni hapo ukiachilia kukosa madawati na walimu  ni maji ambapo inawafanya wanafunzi kushinda mchana kutwa bila kunywa maji hali ambayo ni hatari hivyo katika kikao cha wazazi na walezi waliona kupitisha mchango kila kaya ili kuweza kufanikisha suala la maji na hapo wanachimba  mara baada ya mtaalamu kuja kuthibitisha kuwa maji yapo.

Wazazi na walezi walimu wakikagua shimo ambalo limeanza kuchimbwa ili kuweza kupatikana maji

Hili tanki lilijengwa shuleni hapo kwa msaada wa shilrika lisilo la kiserikali la  OXFARM GB  lenye ujazo wa lita 30,000 lakini halijasaidia kutunza maji sababu  linategemea kuvuna maji ya mvua ikiwa  mvua zenyewe zimekuwa ni kidogo na kufanya maji kutotosheleza pindi likijaa hutumika kwa muda mchache  ikiwa kuna idadi  ya wanafunzi zaidi ya 500 shuleni hapo na maji hutumika sana.

Mwenyekiti wa kijiji cha Amani akiwa shuleni hapo  huku akieleza kuwa kero ya maji imekuwa ni changamoto kubwa shuleni hapo wanafunzi wanapata shida pindi wanapokuwa na kiu wakati mwingine hukimbilia kwenye nyumba za walimu kupata msaada huo hivyo ni wengi hata walimu hawawezi kuwatosheleza kuwapatia maji wanafunzi wote ikiwa hata katika kaya changamoto ya maji ipo kubwa.

Hii ni kamati ya kusimamia uchimbaji wa kisima iliyoundwa na wazazi kwenye kikao cha shule.

0 Response to "WANAFUNZI KUSHINDA BILA KUNYWA MAJI,SHULE YAAMUA KUCHIMBA KISIMA"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.