KANISA la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa
Victoria,Jimbo la Kusini Magharibi limeadhimia kukabiliana na ukosefu wa ajira
kwa vijana wanaokomea kidato cha nne kwa kujenga Shule ya Sekondari ya Ufundi
itakayotoa mafunzo ya stadi za maisha.
Hayo yalielezwa na Mkuu wa Jimbo la Kusini
Magharibi;Mchungaji Daniel Mono katika taarifa aliyoisoma mbele ya Askofu wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa
Victoria,Askofu Emmanuel Makala,wakati wa kuweka Wakfu ujenzi wa Shule ya
Sekondari ya Ufundi ya Agape Lutheran.
Mchungaji Mono alisema ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi ya
Agape utakayojengwa kwa awamu nne utagharimu jumla ya Shilingi 520,623,740/=
ambapo shule hiyo itakuwa msaada mkubwa wa kumudu kujitegemea kimaisha kwa
vijana watakaobahatika kusomea shule hiyo.
Alisema lengo kubwa la kuanzishwa kwa sekondari hiyo ni kuwapatia
wanafunzi masomo ya ziada ya ufundi ambayo ana hakika yatakuwa mkombozi mkubwa
wa kuondokana na maisha ya utegemezi kama walionayo vijana wengi waliokomea
kidato cha nne.
Aidha alisema sekondari hiyo ambayo ni zao la Agape Lutheran
Primary School,kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo imemudu kufaulisha kwa
darasa zima kwa vijana waliomaliza elimu ya msingi hupoteza mwelekeo wao wa
kitaaluma kutokana na kukabiliana na mazingira mapya yanayowabadirisha
kimaadili kutoka waliyozoea ya Kanisa.
Mchungaji huyo alisema matarajio ya Sekondari hiyo ni kuanza January
2016,ambapo mbali na kuwajengea vijana stadi za maisha ili kuondokana na dhana
ya kuajiriwa pia itakuwa msaada mkubwa kwa maendeleo ya Dayosisi kwa
kuongeza uthamani na majengo pindi wanapokuwa katika mafunzo ya
vitendo.
Akifafanua hatua za ukamilishaji wa Sekondari hiyo,awamu itahusu
madarasa manne na ofisi ambayo itakayo gharimu
zaidi ya shilingi millioni mia moja,awamu ya pili itahusu ujenzi wa jiko
na kugharimu Shilingi millioni 150
Awamu ya tatu itakuwa ni kujenga jengo la Utawala na Karakana ya
ufundi itakayogharimu pia Shilingi
millioni 150 huku awamu ya mwisho itakayohusu nyumba za walimu ambazo zitagharimu
Shilingi millioni 120, hivyo kuwaomba wafadhili na marafiki wa kanisa
kujitokeza kuchangia ili kukamilisha kwa wakati sekondari hiyo.
Nae Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania “KKKT”Jimbo
la Kusini Magharibi;Emmanuel Makala aliwaasa watakaosimamia ujenzi huo kuwa
waadirifu na kuhakikisha mradi huo unakuwa na akaunti yake isiyoingiliana na ya
miradi mingine ya Kanisa.
Askofu Makala katika kuhakikisha hilo linafanyika alianzisha
Harambee ya ufunguzi wa akaunti hiyo ambapo zilipatikana kiasi cha Shilingi
Milioni Moja taslimu.
|
0 Response to "KANISA LA KKKT KUNYANYUA VIJANA KATIKA TATIZO LA AJIRA."
Post a Comment