Habari za hivi Punde

JOHN SHIBUDA ATOA KIU YAKE,ASEMA CHADEMA SIO MAMA YAKE, YEYE ATETEA WAPIGA KURA WAKE

Siku chache baada ya Mbunge wa Maswa Magharibi John Shibuda (CHADEMA) kudaiwa kuusaliti Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwa kurudi katika bunge la katiba linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma, na kuwepo taarifa za kufukuzwa ndani ya Chama chake (CHADEMA) Mbunge huyo imeibuka na kusema kuwa amechoswa na Chama hicho.


Chibuda amesema kuwa amechoka kutukanwa, kuitwa msaliti, mnafiki huku akibainisha kuwa kamwe hawezi kuvumilia vitendo hivyo na kubainisha kuwa matusi ambayo yametolewa juu yake sasa yametosha.
Kuhusu kurudi Bungeni.
Akiongelea juu ya taarifa za kurudi bungeni mwanasiasa huyo alisema kuwa taarifa hizo siyo za kweli na hajawahi kuingia ndani ya bunge hilo, bali alipita wakati akitokea Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu
Kuhusu UKAWA.
Akiongelea juu ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) waliogoma kurudi bungeni, Shibuda alisema kuwa umoja huo hauna maslai kwa watanzania ambao alisema asilimia kubwa ni wakulima na wafugaji.
KARENY. Powered by Blogger.