Habari za hivi Punde

VIJANA WAMEONA MAENDELEO YANAYOFANYWA NA MBUNGE WAO

Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa ccm wilaya ya Shinyanga vijijini  Edward Alex akimtunuku hati ya heshima mbunge wa jimbo la SolwaMh  Ahamed Salum kwa mchango wake mkubwa wa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM  kwa kuchangia shughuli za maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Solwa.

Mwenyekiti huyo alisema mbunge Salum ni tofauti na wabunge waliopita kwenye jimbo hilo kwa  kuchangia shughuli za maendeleo.

 Ambapo  katika mfano aliouonyesha ni kutoa magari ya wagonjwa nane katika vituo vya afya na zahanati   mbalimbali  zilizomo kwenye kata hiyo,licha ya mchango huo,  amesema kuwa wananchi wenyewe ni mashahidi ambapo katika ujenzi wa mabweni  hasa zahanati amekuwa akitoa mifuko 200 ya saruji kwa lengo la kufikia hatua ya lenta bila kushirikisha michango ya wananchi  kwenye ujenzi na kisha halmashauri kukamilisha ujenzi huo,

Hata hivyo licha ya kutunikiwa cheti wananchi wa jimbo hilo wamekuwa wakimpa pongezi  katika shughuli za kuwaletea maendeleo hasa kwenye upande wa afya amekuwa ni mkombozi mkubwa katika maisha.

Hivi karibuni katika ziara yake ameweza kutoa mifuko ya saruji 200 kwa kila zahanati inayotakiwa kujengwa zikiwemo wodi za wanawake kwenye vijiji na karibu kata zote za jimbo hilo.
KARENY. Powered by Blogger.