MAMLAKA ya maji safi na utunzaji wa mazingira Tanga
Uwasa mkoani Tanga ina mpango wa kupandisha tozo za maji na kufanyia ukarabati
wa miundombini ili kuondoa uchakavu uliopo uliojengwa tangu ukoloni.
Mkurungezi Mtendaji wa Mamlaka hiyo ya maji safi na
utunzaji wa mazingira wa Tanga Uwasa,Injinia,Joshua Mgeyekwa akizungumza juzi
katika kikao cha wadau kilichofanyika ukumbi wa CCM mkoani hapo alisema lengo
ni kuboresha na kuwaondolea adha inayojitokeza kwa watumiaji wao hasa kwenye
maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la kange.
Pia alitumia nafasi hiyo kuwatoa shaka wadau wa
maji kwamba ni mpango huo wa kuongeza bei ya huduma za maji kwa vipindi vya
miaka mitatu mfululizo unalengo la kuongeza huduma na kasi ya upatikani wa maji
kwenye maeneo mengi hasa yaliyopanuka zaidi.
Mgeyekwa alibainisha kwamba kutokana na kuwa na
ongezeko kubwa la watu na hawana nia mbaya ya kumkomoa mkazi wa Tanga bali ni
kumuhakikishia huduma hiyo ya upatikanji wa maji inapatikana kama
ilivyokusudiwa kwa watumiaji.
Alisema kwamba ili kukabiliana na kuondoa tatizo hilo
kwa wadau wao mamlaka imepelekea kuomba kupandisha tozo hizo za maji sambamba
na ukarabati njia pekee itakayoweza kutoa huduma hiyo kwa tija.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Halima Dendego alisema
mpaka ifikapo June mwaka 2015 itakuwa imejihakikishia kusambaza huduma
ya majisafi na salama kwenye maeneo yote yaliyoko mjini na vijijini
kwa zaidi ya asilimia 99.
Alisema kuwa mpaka sasa miradi ya usambabazaji maji ya
vijiji kumi iliyotoka na fedha kutoka Benki ya dunia ipo katika hatua za mwisho
za kukamilika hali inayotuma uhakika wa huduma hii kuwa itapatika kwa kiwango
kikubwa.
Dendego pia alibainisha kwamba kwa kiasi kikubwa
wilaya ya Tanga haitakuwa na shida ya maji kutoka na mipango iliyopo ya
kuendelea kusogeza huduma hii karibu ikiwemo maeneo ya mjini kulikuwa hakuna
shida ila tabu lilikuwepo vijijini lakini nako litakuwa historia.
Hata hivyo baadhi ya wadau waliohudhulia waliopata
fursa ya kuhudhulia mkutano huo waliipongeza Tanga Uwasa kwa hatua hiyo na
kuitaka kuhakikisha huduma hiyo inakwenda sambamba na tozo watakayoitoa badala
ya kuwa tofauti na walichoahidi kwao.
|
0 Response to "MAMLAKA YA MAJI SAFI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA TANGA KUPANDISHA TOZO LA MAJI."
Post a Comment