RAIS MRISHO JAKAYA KIKWETE.
SHIRIKA lisilo la kiserikali SHIDEFA linalojihusisha na masuala ya sheria limemtaka Raisi Jakaya Mrisho Kikwete kuvunja bunge hilo kama baadhi ya wajumbe wake wa bunge maalumu la kuunda mchakato wa katiba mpya kutorejea bungeni tena kuendelea na mchakato huo ikiwa tayari zimekwisha tumika fedha nyingi.
Shirika hilo ambalo makao makuu yake jijini Dar es salaam limesema kuwa wajumbe wa bunge hilo wameshindwa kuwapatia watanzania katiba mpya na kutumia muda mrefu na fedha nyingi kujadili muundo wa serikali na kuacha kujadili masuala ya msingi ambayo ndiyo kero za wananchi .
Wakiongea na waandishi wa habari wakati wa mdahalo wa kuichambua rasimu ya pili ya katiba Wilayani Bariadi Mkoani simiyu Mwezeshaji Venansi Mazuka kutoka katika shirika hilo alisema kuwa hakuna haja ya wajumbe hao kuendelea na mchakato huo.
Alisema kuwa Raisi kikwete hana budi kuvunja bunge hilo kutokana na wajumbe wa bunge hilo kubishania masuala yasiyo kuwa na msingi wala tija kwa watanzania, huku akibanisha kuwa huduma za jamii, ardhi, pamoja na masula ya kilimo yakiachwa bila ya kujadiliwa.
“tunamtaka Raisi wetu avunje bunge hili..maana wanabishania masula yasiyokuwa na msingi..kero za wananchi siyo serikali tatu au mbili..kero zao ni upatikanaji wa huduma za jamii, umiliki katika ardhi, upatikanaji wa maeneo ya marisho na kilimo..haya wameshindwa kuyajadili” Alisema Mazuka.
Alimtaka kuvunja bunge hilo kisha mchakato kurudishwa kwa wananchi na kupiga kura juu ya muundo wa serikali wautakao ikiwa pamoja na kuundwa kwa tume itakayoongeza masuala ya msingi ya wananchi ambayo ni kero kubwa kwao.
Kama Raisi atafanya hivyo watanzania watapata katiba nzuri na itakayotatua kero mbalimbali zinazowakabili kuliko ilivyo kwa sasa kwa wajumbe hao kuendelea kupoteza muda na kula pesa za walipa kodi kwa kubishania jambo moja bila ya kupata muafaka.
Baadhi ya wananchi waliohudhilia mdahalo huo James Kija na Daniel Kihalo walisema kuwa waliwataka wajumbe hao kuacha kupoteza muda juu ya muundo wa serikali na badala yake kujadili kero zinazowakabili.
|
0 Response to "SHIDEFA IMEMTAKA RAIS KIKWETE KUVUNJA BUNGE MAALUMU LA KATIBA KAMA UKAWA HAWATAKWENDA KWENYE BUNGE HILO."
Post a Comment