|
Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi Nape akiwatambulisha madiwani hao mara baada ya kutangaza kujivua chadema wakiwa jukwaani katika viwanja vya mahakama nguzonane. |
|
Hapa diwani sebastiani Peter akieleza mabaya yote ya chadema mbele ya katibu wa itikadi na uenezi Nape.
|
|
hapa sare za chadema zikiteketezwa kwa moto.
|
MADIWANI wawili wa chama cha demokrasia na Maendeleo (chadema) kutoka manispaa ya Shinyanga wametanganza rasmi kujiuzuru nyasifa hiyo kutokana na madai ya uongozi ngazi ya taifa kuendelea kusikiliza majungu,kudhalilisha baadhi ya viongozi pamoja na kuwaita wahaini au wasaliti katika chama bila kuchambua ukweli na kutotekeleza waliyoyaahidi kwa wanachama wao.
Madiwani hao ni Sebastiani Peter kutoka kata ya Ngokolo na Zacharia Mfuko kutoka kata ya Masekelo kwa pamoja jana waliongea na waandishi wa habari katika ofisi ya naibu meya wa manispaa hiyo huku wakieleza kuwa wanayatamka rasmi maneno mbalimbali yaliyopelekea kujiuzuru kama inshara ya kuwajibika kwa niaba ya makosa yaliyofanywa na viongozi wa kitaifa kwa nyakati tofauti.
Ambapo diwani Sebastiani alisema kuwa kuna sababu tatu zilizopelekea yeye kujiuzuru nafasi ya udiwani na ukatibu wa mbunge vita maalumu , ya kwanza ni mwezi Novemba mwaka 2013 kikundi cha Briged kiliweza kuandika barua kwa katibu mkuu wa chama hicho taifa na kulenga kuwadhalilisha viongozi akiwemo katibu mkoa na wilaya kuwa wamehongwa kiasi cha shilling millioni 90.
“Tuhuma hii leo ninaamini ni tuhuma ya uongo iliyolenga kuwadhalilisha viongozi ambao ni Nyangaki Shilungusheila katibu wa mkoa na Siri yasini mwenyekiti wa wilaya ambapo kimsingi ndio walipotufikisha hapa tulipo,kitendo cha katibu mkuu wa chama kupokea barua hiyo na kushindwa kuifanyia kazi wakati viongozi hawa wamewahi kufungiwa hata kwenye mkutano mkuu wa wilaya jambo hili limenifanya niamini nyumba ya red brigedia wapo viongozi wa kitaifa wanaowaagiza kufanya hayo”alisema diwani Sebastiani Peter.
Alisema jambo la pili ni kutokana na ahadi za mwenyekiti wa taifa Freeman Mbowe kuahihdi chama kitamaliza kujenga nyumba ya marehemu Shelembi aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini na diwani kata ya Masekelo ambapo ahadi aliitoa siku ya mwisho kwenye mazishi ya kiongozi huyo katika viwanja vya shy-com huku mwenyekiti huyo katika kikao kingine alichokuwa akikiongoza kupinga ujenzi wa nyumba hiyo.
Jambo la tatu alisema kuwa tabia ya iliyozuka ndani ya chama hicho ni kuwaita baadhi ya wanachama na viongozi ikiwa ni pamoja kuwadhalilisha kwa kuwabatiza majina mbalimbali ya wasaliti au wahaini wa chama ,waasisi wa kauli hizo ni viongozi hawa wa kitaifa kitendo kinachomfanya aamini kuwa ni uongo ambao hauna tija katika chama.
“Mimi ni miongoni mwa wanachama nitakao kuwa wa mwisho kuamini kama kweli mh Zitto Kabwe ,Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba na wengine ni wasaliti ndani ya chama hiki binafsi najiuliza kama kweli Zitto ni msaliti wa chama na kwa mujibu wa taarifa ya chama zinasema kuwa kutoka mwaka 2008 hadi 2009 aligundulika na kutumiwa na chama cha Mapinduzi (CCM) swali mbona mwaka 2010 waliwezaje kumruhusu kugombea ubunge katika jimbo la Kigoma Kasikazini ?”alisema Sebastian Peter.
Alisema kwa hiari yake kulingana na hayo aliyoyapima ndani ya kichwa chake ameona kuna umuhimu wa kujiuzuru nafasi ya udiwani na ukatibu wa mbunge ikiwa ni njia ya kuwafundisha viongozi namna bora ya kuwajibika kuliko kujionesha mbele ya wananchi kwa mavazi ya kondoo wakati ndani ya mioyo ni mbwa mwitupia sijawa na mpango wa kujiunga na chama chochote nitabaki kuwa katika chama hicho.
Naye diwani wa kata ya Masekelo Zacharia mfuko aliungana na diwani huyo kwa maelezo yake huku akisema kuwa uamuzi wake mpaka kujiuzulu ni kutokana na kuwepo ubabaisha ji ndani ya chama hicho kwani lilikuwepo sakata la mweyekiti wa mtaa kukigawa kiwanja huku kukiwa na kamati ya ugawaji alipokieleza chama walidai kukishughulikia lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea na uongozi wa chama wamekaa kimya ikiwa kimeonekana dhahiri kupingana na sera ya chama hicho kwa kuwatetea wanyonge.
Wote kwa pamoja walikabidhi barua zao za kujiudhuru udiwani katika ofisi za manispaa huku wakimueleza kaimu mkurugenzi Mwanamsiu Dossi taarifa juu ya uamuzi waliouchukua,kuwaombea radhi kama sehemu waliokwaruzana na watendaji wote waliokuwa wakifanya nao kazi kwa pamoja ambapo waliwataka wananchi wa kata zote kuwaona kuwa kitendo walichokifanya sio kwa nia mbaya bali kulijenga taifa lililo makini.
K wa kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 manispaa hiyo ilipata madiwani kumi na saba ambapo chama cha Mapinduzi kilikuwa na madiwani kumi na nne huku chama cha chadema kikiwa na madiwani wanane .
0 Response to "USHUHUDA NDANI YA MIEZI MITANO WAJIVUA GAMBA WAVAA GWANDA"
Post a Comment