Kasulumbayi akiwapa maelekeza madiwani ambao walikuwa wamejiuzuru ambao walikuwa juu ya jukwaa tayari kwa kuongea.
BAADHI YA MAELEZO WALIYOKUWA WAKIYASEMA JUKWAANI
WALIOJIVUA udiwani na uanachama kwa tiketi ya chadema manispaa ya Shinyanga
ambao ni Sebastian Peter kutoka kata ya
Ngokolo na Zacharia Mfuko kata ya
Masekelo kipindi hicho wakijiunga na
(CCM) wameibuka kwenye mkutano wa hadhara wa chadema lengo lao ni
kuwapigia magoti kutaka kurudi ndani ya chama hicho tena.
Umati wa
wananchi waliofurika kujionea kwa
mshangao waliokuwa wakiusikia na mwisho
kujionea watu hao wakipanda
jukwaani ambapo walivua pia sare za CCM
na kuvaa za chadema, kwa nyakati tofauti
walieleza kuwa walitekwa na kushawishiwa
mambo mbalimbali yakiwemo
kupatiwa fedha ili kukisaliti chama hicho.
Mkutano huo
wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya mahakama nguzonane manispaa ya Shinyanga ambapo ulihudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa chama hicho kutoka kanda
ya ziwa akiwemo mbunge wa jimbo la maswa
mashariki mkoa wa simiyu
Slyvester Kasulumbayi Pamoja na katibu mwenezi wa kanda
ya ziwa mashariki Joshua Karando.
“Wanachama
wenzetu tunaomba mtusamehe kwani mambo
haya yalitutokea kwa kushawishiwa na viongozi ndani ya CCM kuwa tukisaliti
chadema leo hii tumekuja mbele zenu tunajutia maamuzi isitoshe hata kadi za
CCM hatukuchukua tumerudi kundini tunaomba mtusamehe tuwe pamoja kama zamani “alisema diwani
Sebastian.
Aidha baadhi ya wafuasi wa chama hicho walionyesha
hasira na kuanza kutaka kuleta vurugu ambapo mbunge Kasulumbayi aliwatuliza huku akiwataka
kusikiliza yale watakayoyaeleza ili kuona unyama unaofanywa na chama cha
mapinduzi kutaka kukivuruga chadema ili
waendelee kushikilia dola,hivyo ujanja wao umebainika na hawa hawana makosa
hakuna budi kuwasikiliza na kusamehe.
Pia Kasulumbayi aliueleza umati huo kuwa suala la kujiuzuru udiwani lilitendeka
kimakosa kwani hata hizo barua hawakuandika wao bali waliandikiwa tena bila
kufuata utaratibu kanuni na sheria kutoka mahakamani ikiwemo vielelezo vyote
vya uchaguzi wa ushindi walioupata viwasilishwe ,kwahiyo inaonekana barua hizo ni batili.
“Hawa
wanahaki zote wametubu wanachadema wenzangu
ninaomba tuwapokee walifanya hivyo kimakosa,tusiwe na hasira kwani kitendo cha kujiuzuru kinatakiwa kipite
mahakamani kwenda kuapa sanjari na vielelezo vyote vinavyotakiwa hivyo bado wanahesabika ni madiwani kwasababu
hawakupitia taratibu kanuni na sheria katika kujizuru kwao”alisema Kasulumbayi.
|
0 Response to "BAADHI YA MANENO WALIYOKUWA WAKITAMKA NA KUTAKA KURUDI CHADEMA."
Post a Comment