Habari za hivi Punde

BAADHI YA MIZANI AINA YA DIGITALI ZIMECHAKACHULIWA NA KUWAPUNJA WAKULIMA.


Wakulima wa kijiji cha Wigelekelo wilayani Maswa mkoani Simiyu wakipeleka pamba yao sokoni.

Pia mzani unaotumika kwa hivi sasa ni mzani aina ya dijiti  ambao unadaiwa kuchakachuliwa na wanunuzi wa zao hilo ikiwa kaimu wakala wa vipimo kwa mkoa wa Shinyanga na Simiyu Juma Chaha alisema kuwa kweli mizani hizo baadhi yao sio waaminifu wanawadanganya wakulima  na kuwapunja ambapo kwa wilaya ya Meatu wakulima wake  walijitahidi kununua mizani yao na kuweza kudhibiti wizi huo,hivyo walikuwa wakiibiwa katika furushi moja lenye kilo mia huondoa kati ya kilo 20 hadi 30 na kumfanya mkulima kupata hasara kubwa.
Hivyo kutokana na changamoto iliyojitokea pia waliomba hata kwenye maeneo mengine kununua mizani zao ili kuweza kuondoa wizi unaofanywa,pia mkulima mmoja kutoka kijiji cha  Zanzuli wilayani Maswa naye alisema kuwa mizani hiyo alishuhudia ikipunja kwani alijaribu kupima uzito katika mizani tofauti akakuta uzito unatofautiana ,licha ya hali hiyo kujitokea wakala wa vipimo wameweka mikakti ya kushirikiana na watendaji wa vijiji na kata wakiwemo madiwani ili kuweza kukomesha  wizi huo.


0 Response to "BAADHI YA MIZANI AINA YA DIGITALI ZIMECHAKACHULIWA NA KUWAPUNJA WAKULIMA."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.