Mwezeshaji kutoka mtandao wa jinsia Tanzania Kenny Ngomuo akiwa katika semina ya waandishi wa habari mkoani Shinyanga march mwaka huu,ambapo alieleza suala la utekelezaji wa masuala mbalimbali ikiwemo elimu,.
Hata hivyo bado asilimia 14 ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka huu
wilayani Kishapu mkoani Shinyanga hawajaripoti shule ikiwa idadi kubwa
ni wasichana huku ikielezwa hakuna sababu yoyote iliyowafanya
wasiripoti ambapo tayari wazazi wanne walifikishwa mahakamani na
kutozwa faini.
Hayo yalisemwa na ofisa elimu vifaa na takwimu
kwa niaba ya ofisa elimu wa sekondari wa halmashauri hiyo Paul
Kasanda wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
ambapo alisema kuwa asilimia hiyo ni sawa na wanafunzi 190 zaidi
wasichana ambao hawajaripoti kwa mwaka huu mpaka sasa.
Alisema
kufikia asilimia 14 ni jitihada zilizofanywa na watendaji wa vijiji na
kata kwani kufikia mwezi march mwaka huu kulikuwa na wanafunzi 525
ambao hawajaripoti sawa na asilimia 22,lakini wazazi walikuwa
wakifuatwa wa watendaji hao huku wakishindwa kutoa maelezo ya kwanini
hawawapeleki watoto wao shule.
“Hizo zote ni jitihada za
watendaji wa vijiji na kata na kufikia asilimia 14, wazazi katika
halmashauri hii hawana mwamko wa kuwasomesha watoto wao hasa wa kike
hata idadi kubwa ya watoto ambao hawajaripoti kuanza kidato cha
kwanza ni wasichana ndio maana hata suala la elimu linazidi kushuka
kwa upande wao ”alisema Ofisa elimu.
Hata hivyo alisema kuwa
kwa mwaka huu, waliojiunga na kidato cha kwanza jumla ni 2141 ikiwa
wavulana ni 1222 na wasichana 919 ikiwa changamoto kubwa ni kuripoti
kwa wanafunzi hao mashuleni na wazazi kutokutoa ushirikiano wa kutosha.
Alisema
kuwa Kati ya shule 25 za kata ,shule ya sekondari Somagedi iliyopo
kwenye kata hiyo imeshika nafasi ya kwanza kiwilaya huku kimkoa
ikishika nafasi ya tano ambapo wanafunzi waliofanya vizuri kumi bora
kiwilaya wasichana ni wawili pekee,wakati huohuo mpaka sasa wanafunzi
wa kidato cha tano walioripoti ni 55 kati ya wanafunzi 83
waliochaguliwa kujiunga na michepuo ya HGK na HGE.
Aidha
alisema kuwa katika michepuo ya HGK wanafunzi waliochaguliwa ni 40
na HGE ni wanafunzi 43 ,Pia kuna walimu 365 na nyumba za walimu 85
ikiwa bado kunachangamoto ya ukosefu wa shule za sekondari kwa kidato
cha tano na sita kwa wilaya nzima ipo shule moja .
Kwa upande
wake diwani wa kata ya Mondo John Ndama alisema kuwa watoto wa kike
wanapaswa kuelimishwa zaidi ikiwa wanauwezo hata wa kuongoza kiwila
na kimkoa kwa masomo yote kinachotakiwa ni uhamasishaji wa wazazi
kuwasomesha watoto wa kike kwa bidii na sio kuwabagua na kuwadhoofisha
kielimu. |
0 Response to "USAWA KWENYE ELIMU KWA WATOTO WA KIKE BADO WILAYANI KISHAPU MKOANI SHINYANGA."
Post a Comment