Habari za hivi Punde

MADIWANI WALIOJIUZURU CHADEMA NA KUJIUNGA CCM WARUDI TENA CHADEMA KWA KUPIGA MAGOTI.

Aliyekuwa diwani wa kata ya Ngokolo Sebasitian Peter akiwa ameshikwa na  walinzi wa chadema ili asipate kipigo baada ya kuwasili kwenye viwanja vya mahakama nguzonane manispaa ya Shinyanga  ambapo  lengo la  kwenda kwenye mkutano huo ni kutaka kuomba msamaha kwa wafuasi wa chama hicho kurudi tena  baada ya kupewa nafasi walieleza kushawishiwa na CCM na kuahidiwa fedha kwa matukio kadhaa watakayoyafanya  jambo ambalo lilionyesha simanzi na huzuni kwa wananchi waliofurika katika mkutano huo ambapo walieandeleo kueleza kuwa bado chama hicho kinampango wa kuvuruga chadema kwa kuanzisha chama cha ACT .
aliyekuwa diwani wa kata ya Masekelo kwa tiketi ya chadema Zacharia Mfuko amewasili katika viwanja vya mahakama nguzonane manispaa ya Shinyanga  huku akiwa amvaa sare ya CCM  kwenye mkutano wa hadhara wa chadema  lengo la kurudi kwake ni kuomba msamaha  ili wamrudishe tena,ambapo alipanda jukwaani akiwa na diwani mwenzie ambaye ni Sebastiani Peter  wa kata ya Ngokolo huku wafuasi wa chama hicho wakijawa na hasira ya kutaka kuleta vurugu.
  wafuasi wa chadema waliokuwa katika mkutano wa hadhara wakipinga kurudishwa kwao ndani ya chama ambapo walidai kuwa tayari walikichafua kwa maneno makali na machafu hivyo hakuna sababu ya kuwarudisha,lakini katika zogo hili mbunge kutoka maswa mashariki Slyvester Kasulumbayi aliwapoza wananchi hao huku akidai kuwa tayari wametubu hata hivyo hawakuwa na kadi za chama cha mapinduzi  na hata zile barua   walizoandika manispaa kujiuzuru ni batili kwani hazikupitia kwenye utaratibu,kanuni na sheria.

KARENY. Powered by Blogger.