WAFANYABIASHARA mkoani Shinyanga
wamelalamikiwa kuwa chanzo cha kuchafua mitaro na makalvati ikiwemo
mama lishe kumwaga maji machafu hali ambayo imesababisha mitaro hiyo
kuziba na kufanya wakala wa barabara tanroad kuingia gharama kubwa ya kuzibua
na kuisafisha .
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake meneja
wa Tanroad mkoa wa Shinyanga Philip Witonde amesema kuwa wafanyabishara wanapouza bidhaa zao
mabaki ambayo ni uchafu hutupwa katika mitaro huku mama
lishe nao humwaga maji machafu hali inayopelekea mitaro hiyo kuziba
kwa haraka.
Witonde amesema kuwa wafanyabishara
wamekuwa ni chanzo cha kuwepo kwa uchafu
katika mitaro kwani hufanya biashara zao kando ya barabara na
mabaki huhifadhi katika mitaro au makalvati isitoshe mama lishe
nao hudiriki kumwaga maji machafu hali ambayo
inawafanya wakala wa barabara kutumia gharama kubwa kuzibua na kuisafisha.
Witonde amesema Suala
la wanaosafisha barabara za manispaa waliokuwa wanafanya
usafi kwakutumia mafagio na kusukuma michanga katika mitaro hilo
waliliona na kumwandikia barua mkurugenzi wa manispaa ya shinyanga
kuwa mchanga sio kuskumwa ndani ya mitaro bali wawe na eneo maalumu ya
kutunza michanga hiyo.
Baadhi ya wananchi wamekuwa sio watunzaji wa mazingira
amesema mara nyingi kumekuwa
wakiweka uchafu wa aina
mbalimbali katika Kalvat na mitaro ,kwa kuona chupa za plastiki
ndani yake kuna haja ndogo,mifuko ya plasiti yenye kinyesi pamoja na
kuchora au kuandika kwa kuchafua kuta za mitaro.
Witonde amesema Suala
la wanaosafisha barabara za manispaa waliokuwa wanafanya
usafi kwakutumia mafagio na kusukuma michanga katika mitaro hilo
waliliona na kumwandikia barua mkurugenzi kuwa mchanga sio
kuskumwa ndani ya mitaro bali wawe na eneo maalumu ya kutunza michanga hiyo.
Baadhi ya wafanyabiashara wamekiri kumwaga maji
machafu katika mitaro ambapo wamesema kuwa kuna wengine sio
wastarabu jambo ambalo wamekuwa wakiambiwa kila siku usafi wa
mazingira kwa kuwa na sehemu ya kuhifadhia maji machafu na taka ngumu pia
kuondokana na magonjwa ya mlipuko.
0 Response to "WAFANYABIASHARA WALALAMIKIWA KUWA CHANZO CHA UCHAFU WA MITARO NA MAKALVAT"
Post a Comment