WANANCHI wa vijiji viwili vya Mwamalili na Seseko kata ya
mwamalili wilayani Shinyanga wamekabidhiwa kwa Jeshi la jadi sungusungu
ilikukamilisha michango ya mradi wa maji utakao sambaza maji safi na salama
katika vijiji hivyo ambao unatoka ziwa Victoria kupitia tenki la maji
(Shuwasa) .
Akilikabidhi Jeshi hilo la jadi kwa wanakijiji hao mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga wakati akizindua mradi wa maji safi na salama
katika vijiji hivyo viwili alisema kutokana na wanakijiji kukaidi agizo la
serikali la sera ya maji ya mwaka 2002, ambayo inasema kila mwananchi
anapaswa kuchangia fedha katika miradi hiyo ya maji kuwa hanabudi kutumia
mamlaka yake
Rufunga alimwambia kamanda wa Jeshi la jadi wa vijiji hivyo
Charlse Makelesia washilikiane na kamati ya maji ya vijiji hivyo viwili
mwamalili na Seseko kuwa watumie njia yeyote ile, ilikufanikisha michango
ya mradi huo wa maji kwa wanakijiji hao, na ifikapo tarehe 30 mwezi huu
michango yote iweimekamilika
Alisema enzi za mwalimu Nyerere wananchi walikuwa kipaumbele
kuchangia miradi ya maendeleo, na baadhi yao ambao walikuwa wanakwamisha miradi
hiyo jeshi la jadi sungusungu lilikuwa likipewa jukumu la kuwashughulikia ,kwa
kuwakamatia mifugo yao au thamani yeyote ile,kwa lengo la kakamilisha michango
na kusukuma gurudumu la maendeleo
Rufuga alisema kutokana na mfumo huo aliokuwa akiutumia
mwalimu Nyerere ambaye pia alikuwa Rais wa kwanza nchini Tanzania katika
kufanikisha maendeleo kwa wananchi na kuinua uchumi wa taifa ,hivyo nayeye
hanabudi kutumia mbinu hiyo katika kuleta maendeleo mkoani shinyanga
Akisoma Taaarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji katika
vijiji hivyo viwili Afisa mtendaji wa kata ya mwamalili Simoni Mpaname alisema
ujenzi huo wa mradi wa maji safi na salama ulitiwa saini tarehe 5 Agousti na
utekelezaji wake ulianza tarehe 12 septemba mwaka jana ambapo kufikia tarehe 31
march mwaka huu, ulitakiwa kukamilika na kughalimu shilingi milioni 538,178,200
Mpaname alifafanua katika kijiji cha mwamalili wananchi
walitakiwa kuchangia mradi huo kiasi cha fedha shilingi milioni 16.9 sawa na
asilimia 2.5 katika kaya 501 ambapo kila kaya ilitakiwa kutoa fedha shilingi
35,000, na kudai kuwa hadi sasa wamechangia laki 469,900 na kubakiwa na deni la
kukamilisha michango hiyo shilingi milioni 16,5.
Alisema katika kijiji cha Seseko wananchi walitakiwa
kuchangia Shilingi milioni 9 kwa kaya 360 ambapo kila kaya ilitakiwa kutoa
fedha shilingi 30,000 na kudaiwa kuwa hadi sasa wamechangia laki 865,000 huku
wakibakiwa na deni la kukamilisha michango hiyo shilingi 8,135,000 hali ambayo
imechangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha mradi huo wa maji safi na salama katika
vijiji hivyo viwili.
Akielezea sababu za wananchi kushindwa kuchangia fedha hizo
mwenyekiti wa kamati ya maji katika vijiji hivyo Elisha Mahalala alisema sababu
kubwa ni wananchi kuchanganya masuala ya maendeleo na siasa, kuwa Mmbuge wa
jimbo la shinyanga Steven Masele aliwaahidi kuwaletea maji, hivyo hawawezi
kutoa fedha hizo huku baadhi yao wakisingizia wanakabiliwa na njaa.
0 Response to "JESHI LA JADI LAPEWA DHAMANA YA KUSIMAMIA MICHANGO YA MRADI WA MAJI"
Post a Comment