HAKIMU mkazi mwandamizi mfawidhi mkoa wa shinyanga John Chaba ameiomba serikali mkoani
shinyanga kukamilisha ujenzi wa jengo la mahakama kuu kanda ya ziwa
linalojengwa kwa haraka ilikurahisisha uendeshaji wa kesi hali ambayo
itasaidia kesi nyingi kusikilzwa kwa wakati.
Hakimu Chaba alisema hayo kwenye siku ya madhimisho ya
sheria nchi ambapo kimkoa yalifanyika mjini shinyanga katika viwanja vya
mahakama ya hakimu mkazi kuwa mahakimu mkoani humo wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali moja kuu ikiwa ni upungufu wa majengo ya mahakama ya kuendeshea kesi
na hivyo kufanya kesi nyingi kurundikana mahakani
Alisema endapo jengo la mahakama ya Rufaa kanda ya ziwa
mkoani hapa litakapokamilika litasaidia kuepusha mrundikano wa kesi mahakamani
kwani kesi nyingi hupangiwa tarehe kila mara kutokana na uhaba wa majengo ya
mahakama kuendeshea kesi hizo pamoja na upungufu wa mahakimu kwani kesi
nyingine zinakuwa hazijamaliza upelelezi
‘’Tumekuwa tukukabiliwa na changamoto mahakimu katika
utendaji wetu wa kazi uhaba wa majengo ya mahakama,miundombinu kuwa
mibovu,uchakavu wa majengo,ufinyu wa bajeti ya fedha za mahakama, wadau
kutoshiriki kikamilifu, na jengo kuu la mahakama ya rufaa ndilo kwa asilimia
kubwa tulikuwa tunategemea kuendeshea kesi hizo “alisema hakimu Chaba
Alisema jengo hilo lilianza kujengwa mwaka 2008 mapaka hivi
sasa halijakamilika na hivyo kuwapa wasiwasi juu ukamilifu wa mahakama hiyo,na
aliongeza kuwa mbali na kesi hizo pia huwaingizia ghalama wananchi
kusafiri kwenda kusikiliza kesi za Rufaa mkoani Tabora
Upande wake mgeni
Rasmi mwanasheria kutoka ofisi ya mkoa
shinyanga Lightness Tarimo akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa aliwataka
mahakimu hao kufanya kazi kwa weledi ,ufanisi pamoja na kufuata misingi ya
sheria na katiba ya nchi
Katika hatua nyingine viongozi wa madhehebu mbalimbali
waliohudhuria maadhimisho hayo kwanyakati tofauti wakitoa sara zao kuwaombea
mahakimu waliwataka kusimamia sheria ipasavyo na kuacha kupindisha haki
huku wakiwataka kuhukumu mtu kutokana na kosa alilotenda
0 Response to "HAKIMU AELEZA UFINYU WA MAHAKAMA UNASABABISHA UENDESHAJI WA KESI KUCHELEWA."
Post a Comment