WAFUGAJI wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wametakiwa kubadilika kufuga mifugo wenye uwezo wa
kuchukua muda mfupi wa kukomaa na kuweza kuingia sokoni, pia kulichukulia kama
zao la biashara kutokana na hali ya hewa
ya ukame katika wilaya hiyo ikiwemo
changamoto ya kukosa maeneo ya malisho pamoja na majosho.
Hayo yalisemwa na waziri wa maendeleo ya mifugo na
uvuvi Titus Kamani katika ziara yake aliyotembelea wilayani humo
huku akiwaeleza wataalamu na mkuu wa wilaya hiyo Wilson Nkhambaku kuwa wakulima
wamekuwa wakilima kila eneo na kufanya wafugaji kukosa maeneo ambapo inatakiwa
wapatiwe elimu hiyo na kuweza kuepusha migogoro inayoendelea kati ya wakulima
na wafugaji nchini.
Kamani alisema kuwa wafugaji wamekuwa wakikumbwa na
changamoto nyingi ya kufuga mifugo mingi
yenye kuchukua muda mrefu kukua na kuingia sokoni ambapo kumekuwa na uhaba wa meneo ya malisho
kwao huku akisikitishwa na taarifa ya mkuu wa wilaya hiyo kuwepo kwa majosho 27
ila yanayofanya kazi ni majosho matatu.
“Wafugaji lazima wabadilike
wanauwezo wa kufuga mifugo yenye
kukomaa kwa muda wa mwaka mmoja na nusu
huku mbuzi akiweza kukomaa kwa muda wa miezi sita na kuingia katika soko la
biashara, na kuichukulia kama zao lao
kuu kulingana na hali ya hewa ya ukame kwa mazao mengine kushindwa kustawi
vizuri”alisema Waziri Kamani
Alisema kuwa sekta ya mifugo imekuwa haionekani kuingizia
taifa pato la kutosha kama madini ikiwa
barani Afrika nchi ya Tanzania inaongoza kwa kuwa na mifugo mingi zaidi ya
millioni 20, mbuzi millioni 15 na kondoo
ni millioni 7 ambapo sekta
hii imekuwa ikilalamikiwa ,wafugaji
wamekata tamaa na kujichungia wanavyotaka bila kujikita kuboresha suala hili, hakika umasikini hauta ondoka.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Nkhambaku alibainisha kuwa asilimia 88.1 ya wakazi wa
wilaya hiyo wanategemea uchumi wa kutoka kwenye kilimo na mifugo ikiwa asilimia
27 wanajihusisha na mifugo pekee ambapo
kumekuwepo na ongezeko la mifugo isiyokuwa na tija kwa mwaka 2007 kulikuwa na
ng’ombe zaidi ya laki mbili na mikakati
iliyopo ni uhimilishaji madume na majosho yaliyopo 27 yanayofanya kazi ni
matatu.
Ambapo alisema kuwa kupitia uhimilishaji madume kwa mwaka
2012 kwa ng’ombe 200 na kuweza kupata
ndama zaidi ya 10 katika vijiji sita ikiwa imetenga
shilingi millioni 16 kwa lengo la kukarabati majosho 10 na shilingi millioni 71
kwaajili ya kununua madume bora 100 na kuamua kubadilisha mfumo wa ufugaji pia
changamoto ya hali ya hewa ukame kwa kupata mvua wastani Mm 506 hadi Mm 567 na
uhaba wa maji.
“Wilaya hii imekuwa na migogoro ya ardhi na mipaka kutoka
kwa wakulima na wafugaji hasa kwenye vijiji vya Buzinza na Maghalata pia mgogoro mwingine ni kati ya wilaya ya
Kishapu na Igunga,pia kumekuwepo na uhimilishaji
wa ng’ombe 200 katika vijiji vitano na Majosho kwenye vijiji sita mikakati
iliyopo majosho kumi kukarabatiwa na
kubadilisha mfumo wa ufugaji ili waweze kunufaika wafugaji”alisema Nkhambaku.
Hata hivyo baadhi ya wafugaji wilayani humo akiwemo Jilunde Ndalu
alisema kuwa changamoto kubwa imekuwa ya uhaba wa maji na malisho hali inayowafanya kuhama hama kwa
kutafuta maeneo pia mifugo imekuwa na afya dhaifu kwa kukosa malisho hasa kipindi cha kiangazi angalau masika nyasi zinakuwepo mbugani na
unafuu wa malisho kiasi.
0 Response to "WAFUGAJI WILAYANI KISHAPU WATAKIWA KUBADILISHA MFUMO WA UFUGAJI KUTOKANA NA HALI YA HEWA KUWA YA UKAME"
Post a Comment