Habari za hivi Punde

HAKIMU AELEZA UFINYU WA MAHAKAMA UNASABABISHA UENDESHAJI WA KESI KUCHELEWA.






HAKIMU mkazi mwandamizi mfawidhi mkoa wa shinyanga John  Chaba ameiomba serikali  mkoani  shinyanga kukamilisha ujenzi wa jengo la mahakama kuu kanda ya ziwa linalojengwa kwa haraka  ilikurahisisha uendeshaji wa kesi hali ambayo itasaidia kesi nyingi kusikilzwa kwa wakati.

Hakimu Chaba alisema hayo  kwenye siku ya madhimisho ya sheria nchi ambapo kimkoa yalifanyika mjini shinyanga katika viwanja vya mahakama ya hakimu mkazi kuwa mahakimu mkoani humo wanakabiliwa na changamoto mbalimbali moja kuu ikiwa ni upungufu wa majengo ya mahakama ya kuendeshea kesi na hivyo kufanya kesi nyingi kurundikana mahakani


Alisema endapo jengo la mahakama ya Rufaa kanda ya ziwa mkoani hapa litakapokamilika litasaidia kuepusha mrundikano wa kesi mahakamani kwani kesi nyingi hupangiwa tarehe kila mara kutokana na uhaba wa majengo ya mahakama kuendeshea kesi hizo pamoja na upungufu wa mahakimu kwani kesi nyingine zinakuwa hazijamaliza upelelezi

‘’Tumekuwa tukukabiliwa na changamoto mahakimu katika utendaji wetu wa kazi uhaba wa majengo ya  mahakama,miundombinu kuwa mibovu,uchakavu wa majengo,ufinyu wa bajeti ya fedha za mahakama, wadau kutoshiriki kikamilifu, na jengo kuu la mahakama ya rufaa ndilo kwa asilimia kubwa tulikuwa tunategemea kuendeshea kesi hizo “alisema hakimu Chaba

Alisema jengo hilo lilianza kujengwa mwaka 2008 mapaka hivi sasa halijakamilika na hivyo kuwapa wasiwasi juu ukamilifu wa mahakama hiyo,na aliongeza kuwa mbali na kesi hizo pia huwaingizia ghalama wananchi  kusafiri kwenda kusikiliza kesi za Rufaa mkoani Tabora

 Upande wake mgeni Rasmi mwanasheria kutoka  ofisi ya mkoa shinyanga Lightness Tarimo akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa aliwataka mahakimu hao kufanya kazi kwa weledi ,ufanisi pamoja na kufuata misingi ya sheria na katiba ya nchi

Katika hatua nyingine viongozi wa madhehebu mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo kwanyakati tofauti wakitoa sara zao kuwaombea mahakimu  waliwataka kusimamia sheria ipasavyo na kuacha kupindisha haki huku wakiwataka kuhukumu mtu kutokana na kosa alilotenda

0 Response to "HAKIMU AELEZA UFINYU WA MAHAKAMA UNASABABISHA UENDESHAJI WA KESI KUCHELEWA."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.