ZAHANATI inayomilikiwa na mtu binafsi katika kijiji cha songambele kata
ya Salawe wilayani Shinyanga imefungwa na wataalamu wa afya
kutoka mkoani hapa kutokana na kukosa vigezo vya kuwa zahanati
babala ya duka
la madawa kama ilivyokusudiwa huku daktari msimamizi wa wakimkataa
kwa kukosa sifa, ambapo ilikuwa ikitoa huduma mbalimbali za
matibabu kama vile upimaji wa damu,malaria na uzalishaji wa
mama wajawazito.
Zahanati hiyo imefungwa mwezi januari mwaka huu,ambapo mmiliki wake dkt Daniel
Emanuel aliwaeleza waandishi wa habari kuwa zahanati imepata
usajili mwaka 1994 na kuanza kutoa huduma katika kijiji
hicho ambapo kwa siku alikuwa akihudumia wagonjwa zaidi ya
kumi.
Dkt Emanuel alisema kuwa haelewi sababu za
kufungwa kwa zahanati hiyo kwani walifika wataalamu wa afya kutoka
mkoani na kumueleza kuwa hana wataalamu wa kutosha kuendesha
zahanati hiyo huku wakimkataa msimamizi wa zahanati kuwa hana
sifa na hakuna wataalamu wakutosha.
Ambapo ameeleza kuwa zahanati hiyo ilikuwa na wafanyakazi
watano akiwemo msimamizi ambaye walimkataa kwa madai hana sifa ya kusimamia
zahanati hiyo sanjari na kukagua vipimo vilivyomo ndani ya maabara huku
wakiondoka na vifaa hivyo.
“Mimi nashangazwa na wataalamu kutoka serikalini
kuja kunifungia kwani wataalamu ninao wa watano , wakiwemo
wauguzi na daktari wenye sifa , kisheria zahanati inatakiwa
hata wakiwa wawili inatosha kwa sababu huduma
zinazotolewa sio nyingi ,ila msimamizi wa zahanati wamemkataa
kuwa hana sifa kipimo cha maabara wamekichukua na kuondoka nacho.”alisema
dkt Emanuel.
Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho Mhoja
Shija na James Membe walisema kuwa zahanati hiyo ilikuwa msaada mkubwa
kwa watu ndani ya kijiji hicho na kuwa kimbilio mara
wanapougua kwa kupata huduma ya
haraka japo kwa malipo tofauti na zahanati ya serikali
mara nyingi zimekuwa na changamoto nyingi hasa za
ukosefu wa dawa .
Naye mwenyekiti wa halmashauri hiyo Ngassa Mboje alisema kuwa kufungiwa kwa zahanati hiyo imetokana na
kukosa sifa ikiwemo kwenye orodha ya
usajili kama zahanati haimo ambapo
inaonekana mpaka sasa ni duka la uuzaji
wa dawa na kutofuata utaratibu wa sheria za afya.
Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya hiyo dkt
Archie Hella alisema kufungiwa kwa zahanati hiyo
kutokana na kushindwa kufikia vigezo vya kuwa zahanati ambapo
ilibainika kuwa haina wataalamu wenye sifa wa kuweza kutoa
huduma hiyo kwa watu pia ilikuwa ikiendesha kinyume cha sheria na
taratibu za afya.
0 Response to "ZAHANATI YAFUNGWA KWA KUKOSA VIGEZO."
Post a Comment