MKOA Wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa sita nchini
ambayo inakabiliwa na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama
Mjamzito kwenda kwa mtoto na kufikia asilimia 7.3
Hayo yamelezwa na Dkt Hamis Kulemba ambaye ni Mratibu wa kuzuia magonjwa ya ngono na Ukimwi mkoa wa Simiyu wakati wa sherehe za uzinduzi wa mpango wa kutokomeza maambukizi mapya ya VVU kwa mtoto kutoka kwa mama mkoani humo
Hayo yamelezwa na Dkt Hamis Kulemba ambaye ni Mratibu wa kuzuia magonjwa ya ngono na Ukimwi mkoa wa Simiyu wakati wa sherehe za uzinduzi wa mpango wa kutokomeza maambukizi mapya ya VVU kwa mtoto kutoka kwa mama mkoani humo
Dkt Kulemba alisema mpango huo ni mwitikio wa mpango wa kitaifa wa utokomeza VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kutoka asilimia 15 ya mwaka 2012 hadi kufikia chini ya asilimia nne ifikapo 2015.
Alisema mpango huo unalenga kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa asiliami 50 miongoni mwa wanawake wenye umri wa kuzaa kati ya miaka 15 hadi 49 na kuongeza na kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango miongoni mwa akina mama wenye maambukizi ya VVU.
"Aidha mpango huu utaongeza upatikanaji wa tiba ya ARV kwa akina mama wajawazito na wanaonyonyesha na kwa watoto walioambukizwa VVU,"
alisema.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Dkt Matoke Muyenjwa alisema kwa kupitia mpango huo akina mama wajawazito na watoto wote walioambukizwa VVU wataanzishiwa dawa za ARV ambazo wataendelea kuzitumia kwa maisha yao yote.
Alisema mpango wa kutoa dawa za kuzuia maambukizi ya VVU uanze, maambukizi ya VVU toka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto yanapungua mwaka hadi mwaka.
Mwaka 2013 akina mama wajawazito 36,966 walipimwa VVU ambapo kati yao wajawazito 701 walionekana na VVU sawa na asilimia 2 watoto waliozaliwa na mama wenye maambukizi ya VVU walikuwa 895 na kati ya hao watoto 66 sawa na asilimia 7.3 waligundulika kuwa na maambukizi ya
VVU'alisema. .
Aliongeza kueleza kuwa wanawake wajawazito wakijifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma serikali itawahakikishia usalama na watapewa elimu ya namna ya kuzuia maambukizi kwa mtoto
0 Response to "MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU KUTOKA KWA MAMA MJAMZITO KWENDA KWA MTOTO YAFIKIA ASILIMIA7.3 MKOANI SIMIYU"
Post a Comment