Habari za hivi Punde

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AKUTWA AMEJINYONGA HUKU AKIACHA UJUMBE MZITOMWALIMU  wa shule ya msingi Mwang’osha kata ya nyamalongo wilaya ya shinyanga  mkoani hapa Christipian Mafuru (24) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani katika choo kilichopo nyumbani kwake huku akiacha ujumbe mzito uliotia simanzi.

 Mwalimu mkuu wa shule hiyo Frida Maleko aliwaeleza waandishi wa habari kuwa  marehemu aligundulika akiwa amejinyonga juzi majira ya saa tisa na nusu alasiri mara baada ya kutoonekana shuleni kwa mda mrefu.


Ambapo mwalimu huyo  alichukua jukumu la kumpigia simu  marehemu bila ya mafanikio na kuamua kuondoka na walimu wenzake kwenda nyumbani kwake na kukuta mlango umefungwa huku simu ikiita ndani bila ya kupokelewa

Alisema hali hiyo iliwatia mashaka na hivyo kujukua jukumu la kuvunja dirisha la nyumba hiyo na mara baada ya kufanikiwa kuingia ndani hawakukuta mtu bali walikuta na ujumbe wa maneno( Barua) mezani uliokuwa umeandikwa na marehemu ukisomeka kuwa ‘’Msongo wa mawazo umenilazimu nifanye hivi, poleni sana walimu wenzangu,samahani wazazi wangu,kwa heri mwanagu Ray” hali ambayo iliwatia hofu kubwa.

‘’Marehemu aliajiriwa mwaka jana hapa shuleni kwetu na alikuwa mchapakazi na aliomba zamu zote za walimu azifanye yeye iliapate uzoefu wa kazi, lakini nilishituka kwakutomuona muda mrefu shuleni hapo ikabidi nimpigie simu nimuulize kulikoni hujafika shule leo lakini simu haikupokelewa”alisema mwalimu mkuu

Aliongeza kuwa mara baada ya kuona mlango umefugwa kwa ndani nilipiga simu yake tena ambapo ilikuwa inaiita kwa ndani bila ya kupokelewa na ndipo tuliposhauriana na walimu wenzangu tuvunje dirisha baada ya kuingia ndani tukakuta ujumbe wa barua  hiyo.

 Baada  ya kumtafuta kila mahali ambapo walifanikiwa kumkuta ndani ya choo huku akiwa tayari amekufa kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani hali ambayo iliwaogopesha na kuamua kutoa taarifa kwa jeshi la polisi

 Kwa upande wa kamanda wa jeshi la polisi mkoani shinyanga  Evarist Mangalla alithibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisema chanzo cha  kifo hicho ni msongo wa mawazo wa mwalimu huyo kutokana na barua aliyoandika yeye mwenyewe kwa mkono wake na kutia saini na hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na jeshi la polisi juu ya kifo hicho
KARENY. Powered by Blogger.