HATIMAYE kiwanda cha
kusindika nyama cha Triple ‘S’
kilichopo manispaa ya Shinyanga kimeanza
kuingia mkataba kwenye vikundi vidogo vidogo vya wafugaji vilivyopo mkoani hapa kwa lengo la
kuwanyanyua kiuchumi huku kikiwa
kimekwisha pata soko la uuzaji nyama hizo nchi ya Uarabuni.
Hayo yalisemwa na mmiliki wa
kiwanda hicho Salum Seif mbele ya waziri wa maendeleo ya mifugo na
uvuvi Titus Kamani wakati wa ziara yake mkoani humo na
kutembelea kiwanda hicho huku akieleza kuwa
anatarajia kukifungua na kuanza
kazi mwezi Marchi mwaka huu ikiwa ataanzia na ng’ombe 50.
Alisema wamekuwa na
maongezi katika vikundi vidogo vidogo vya
ufugaji mkoani hapa lengo kuwanyanyua wafugaji hao kiuchumi ,hawakutaka
kuwatumia madalali katika minada ambao
wamekuwa wakiwapunja wafugaji na kujinufaisha wenyewe hivyo wameona watumie mwanya wa vikundi nao
wapate faida kubwa na kuondokana na unyonywaji.
“Kiwanda hiki kinauwezo kwa kuchinja ng’ombe 250 hadi 300
kwa siku ila kwa kuanza tutaanzia ng’ombe 50 pia tumekwisha ongea na
wasambazaji kwenye masoko wa nyama hiyo
pindi itakapo kuwa tayari,tumeongea na nchi ya uarabuni wamedai wako tayari kununua nyama yote
inayotoka ndani ya kiwanda hiki ikiwa tangu mwaka 2008 nimekuwa nikikifanyia ukarabati sasa kuanza
rasmi ni mwezi Marchi mwaka huu.”alisema Self.
Naye waziri Kamani alisema kuwa lengo la kuwepo kiwanda
hicho nikutaka watanzania kuacha kuagiza bidhaa hiyo kutoka nje na pindi kitakapo kuwa tayari kitawezesha hata mikoa mingine kuleta mifugo
yao ambapo barani Afrika Tanzania
imeonekana kuwa na mifugo mingi zaidi ya millioni 40 ikiwemo mbuzi na kondoo.
Aliwataka wafugaji watumie kiwanda cha nyumbani kinachoweza kuchukua mifugo , ila changamoto
kubwa iliyopo ng’ombe wa hapa nchini hawana ubora wa kuingia kwenye ushindani wa soko la nyama
hivyo inatakiwa wafugaji wabadilike kwa mfumo wa ufugaji na kuwa wa kibiashara ili waweze kunyanyua uchumi wa mkoa na mtu mmoja mmoja.
Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Annarose Nyamubi alimtaka mwekezaji huyo kuwaelimisha wananchi walio kandokando ya kiwanda hicho kwa kupitia
afisa maendeleo ya jamii kwa
kutenga maeneo ya kuendeleza shughuli
zao ili kuweza kuepusha migogoro isiyokuwa yalazima pia wafugaji wapate
kuelimishwa ili waweze kunufaika na kiwanda hicho.
Wafugaji kutoka kata
ya Samuye wilayani humo Mhoja Masengwa alisema kuwa kiwanda hicho kabla ya kuanza kununua mifugo
kwa wakulima watoe elimu ya mifugo gani wanayohitaji kama inakubalika waweze
kuingia katika soko isije badaye
ikaonekana kuwanyima kipaumbele wenyeji
na kujikita katika wafugaji kutoka nje na kuonekana ndio wenye ubora zaidi.
Historia ya kiwanda hicho kilijengwa mwaka 1975 hakikuwahi kufanya kazi hata siku moja ambapo mwaka wa 2008 kiliweza kupata
mwekezaji kutoka kampuni hiyo na kuanza
kukifanyia ukarabati wa kuondoa vifaa
vilivyokuwa chakavu ikiwa kinatarajiwa
kuweka historia mkoani Shinyanga kwa kuanza kazi marchi mwaka huu.
0 Response to "KIWANDA CHA KUSINDIKA NYAMA CHAANZA MAZUNGUMZO NA WAFUGAJI KWENYE VIKUNDII"
Post a Comment