KITUO cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino)
kilichopo Buhangija katika manispaa ya Shinyanga bado kinakabiliwa na upungufu
mkubwa wa chakula, vyandarua,vifaa vya kufanyia usafi pamoja na
upungugufu wa vitanda ambapo kuna watoto 258 huku kukiwa na vitanda 60.
Hali hiyo ya ukosefu wa vitanda imewalazimu kulala kila
kitanda watoto wanne wanne ambavyo pia ni vitanda vya dable deca vinavyofaa
kulaliwa na watoto wawili tu.
Hayo yalibainishwa juzi kwenye sherehe za kutimiza miaka 37
ya Chama cha mapinduzi (CCM) wakati umoja wa vijana UVCCM wilaya ya Shinyanga
mjini walipokuwa wakiazimisha sherehe hiyo katika kituo hicho
ambapo walifanya usafi katika maeneo hayo walifua nguo za watoto hao, walipanda
miti pamoja na kutoa msaada wa chakula.
Akizungumza katika sherehe hiyo mkuu wa kituo hicho Britoni
Mduma alisema bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya chakula kwani sasa hivi
wana mahindi tu lakini hawana mboga, maharagwe mafuta pamoja na chakula cha
kubadilisha.
“Vijana hawa wanakula chakula cha mlo mmoja tu ambacho ni
ugali mchana na jioni kwa sababu hatuna chakula cha kuwabadilishia hivyo
tunaiomba serikali iwakumbuke watoto hawa, pamoja na wahisani wengine
mbalimbali waguswe ili na wenyewe waweze kubadilisha chakula pamoja na
kuwaongezea vitanda kwani wanalala kwa kubanana sana”alisema Mduma.
Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa vijana UVCCM wilaya
ya Shinyanga mjini Abubakari Mkadam alisema kuwa wameona vyema kuazimisha
sherehe hizo za miaka 37 ya CCM kwa kutembelea katika kituo hicho kwa
kuwasaidia kufanya usafi wa mazingira, kupanda miti kufua nguo pamoja na kutoa
msaada wa chakula ,kwa lengo la kushiriki nao sherehe hizo za kuzaliwa kwa CCM.
Aliongeza kuwa sherehe nyingi za CCM zimekuwa ziki
adhimishwa kwa kufanya mikutano mbalimbali ya wananchi ambapo kwa mwaka huu
(2014) wameona wafanye tofauti kwa kuwa tembelea vijana wenzao ambao huishi
katika mazingira magumu na hatarishi
Naye mjumbe wa Halmashauli kuu ya umoja wa vijana CCM
wilaya Lucas Jeremia alisema kuwa jamii inapaswa kutambua uwepo wa watoto
hao kwani wanaishi maisha ya tabu sana na yamashaka hivyo inatikiwa kuwakumbuka
kwa kuwapa misaada mbalimbali
Aidha mmoja wa watoto hao walemavu wa ngozi Semen Deusi
aliwashukuru vijana hao wa UVCCM kuwatembela katika kituo hicho na kukishukulu
chama tawala kwa kuwakumbuka katika siku za maadhimisho yake huku akitoa wito kwa
vyama vingine kuiga mfano huo
“Tunashukuru chama cha umoja wa vijana CCM kuja kuazimisha
sherehe katika kituo chetu kwani haijawahi kutokea na tunaomba waendelee
kufanya hivyo hata katika sherehe zingine pamoja na taasisi binafsi kwa
kutusaidia licha ya kumaliza matatizo yetu hata kutupunguzia tu inatosha”
alisema Mtoto huyo mlemavu
0 Response to "UVCCM MANISPAA YA SHINYANGA WAIBUKA SHEREHE ZA KUADHIMISHA MIAKA 37 KUSAIDIA WATOTO WALEMAVU"
Post a Comment