BAADHI ya mashabiki wa timu ya mpira wa miguu manispaa ya shinyanga akiwemo naibu waziri wa nishati na madini Steven Masele kunusurika na wengine kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao kutokana na vurugu zilizozuka ndani ya uwanja wa Kambarage ambapo jeshi la polisi
lilianza kurusha mabomu ya machozi .
Mabomu hayo yaliweza kuleta madhara kwa mashabiki ambapo mama mwenye ujauzito wa miezi nane aliyefahamika kwa jina la Johari Abdallah (23) mkazi wa ngokolo amelazwa kwa presha katika hospitali ya mkoa na mwamuzi Steven Lutaselwa aliyekuwa jukwaani akiangalia mpira alijeruhiwa vibaya sehemu za makalio na hali yake bado ni mbaya yuko chumba mahututi.
Katika mechi iliyokuwa ikichezwa na timu za Stand united ya Shinyanga pamoja na timu ya Polisi Mara zilikuwa zikiminyana
siku ya jumamosi katika uwanja wa kambarage huku mgeni rasmi akiwa naibu waziri huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini naye alipigwa mabomu mawili ya machozi yaliyotupiwa mezani na kuamuru kwenda kujificha kwenye chumba cha mazoezi (GYM)
Ilionyesha kuwa mabomu hayo yalipigwa baada ya mchezo kumalizika huku stendi united ikishinda kwa goli moja kwa bila katika mchezo huo,ambapo mwamuzi aliyekuwa akichezesha pembeni alivamiwa na kiongozi kutoka
timu ya polisi Mara kutaka kumpiga huku polisi waliokuwepo ndani ya
uwanja huo wakitazama bila kwenda kutoa msaada wowote.
Hata hivyo vurugu zilianza baada ya kocha msaidizi wa timu ya Polisi Mara kwenda kupeana mkono na kocha wa timu ya Stend united ndipo alipofika eneo la kikosi cha timu hiyo kabla ya kupeana mkono alimnasa kibao kocha wa timu ya stend united ambapo kiongozi wa nidhamu wa timu hiyo Said Mponda alipokwenda kuamua alianza kushambuliwa na polisi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu (Shirefa) mkoani Shinyanga Benesta Lugolla alisikitishwa na kitendo cha polisi kutumia
nguvu kubwa kuchambulia mashabiki waliokuwa wamekaa jukwaa kuu akiwemo
na mgeni rasmi kitendo ambacho kimeonekana ni udhalilishaji hata kwa
naibu waziri huyo ikiwa chama kiliomba askari wachache cha kushangaza waliokuja ni wengi.
Baada ya kuhojiwa na waandishi wa habari naibu waziri Masele alieleza kuwa aliiomba shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kuangalia upya timu za majeshi hasa polisi kwani wamekuwa chanzo cha matatizo katika viwanja vingi ,pia wamekuwa wakilindana na kutotaka kushindwa inaonekana mpango huu ulikuwa umesukwa muda mrefu..
0 Response to "TIMU YA STENDI UNITED NA POLISI MARA ZALETA KIZAA ZAA UWANJA WA KAMBARAGE MKOANI SHINYANGA "
Post a Comment