MTOTO Said Joshua (12) aliyekatwa
koromeo kwa kutumia kisu na baba yake mzazi huko wilayani Kahama mkoani
Shinyanga amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa
ya Bugando jijini Mwanza.
Mtoto huyo ambaye alichinjwa na baba yake aitwaye
Joshua Salvatory (37),fundi baiskeli akiwa nyumbani kwake usiku wa kuamkia
tarehe 4 mwezi huu katika kitongoji cha Majengo Kaskazini,kata ya
Majengo,tarafa ya Kahama mjini mkoani Shinyanga
amefariki dunia jana jioni majira ya saa kumi kasorobo.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Kitongoji cha Majengo Kaskazini Noel Makula Museven alisema mtoto huyo alifariki akiwa Bugando alikokuwa amelazwa kwa matibabu zaidi mara baada ya hali yake kuwa mbaya katika hospitali ya wilaya ya Kahama alikokuwa anapatiwa kutokana na koromeo lake kukatwa lote kwa kisu na baba yake kutokana na kile kilichodaiwa kuchoka kumtibu maradhi yaliyokuwa yanamsumbua mara kwa mara.
Kitendo cha kuchinjwa kwa mtoto Said Joshua na
hatimaye kusababisha kifo chake kimeibua mambo mengi huku baadhi ya wakazi wa
Kahama wakidai kuwa pengine kitendo hicho kinatokana na imani za kishirikina
kwa madai kuwa mtuhumiwa alikuwa amemtoa sadaka mwanae kwa waganga ili kupata
utajiri.
Baadhi ya wananchi walisema Salvatory amefanya kitendo
hicho kwa lengo la kulipa mchango wa Freemason na kwamba alitaka kuchangia damu
ya mtoto mdogo akakataliwa.
“Ndugu mwandishi haya mauaji wengi wanayahusisha na
imani za kishirikina kwani hivi sasa jamii ya wana Kahama inakabiliwa na balaa
la kuamini vitu na mambo yasiyo na msingi kama lile la kubaini wachawi na imani
ya Freemason ambayo haijulikani hata ilikotoka wala msingi wake”,alisema mkazi
wa mmoja wa Kahama.
Naye mwenyekiti wa Kitongoji cha Majengo Kaskazini Noel Makula
Museven alisema kifo cha mtoto huyo kinatokana na imani za kishirikina kwani
kumekuwepo na taarifa kuwa Joshua Salvatory alikuwa amemtoa sadaka
mwanaye Said Joshua kwa waganga ili awe tajiri.
“Kitendo cha kufirisika kwa mtuhumiwa na mtoto
kuendelea kuugua kifafa,nadhani ndicho kimemfanya ammalize tu mtoto
huyu,taarifa za kwamba ana matatizo ya akili siyo kweli kwani mtuhumiwa kwanza
na mwizi mzuri tu,amefikishwa polisi siku za nyuma kwa wizi,sasa inakuwaje mtu
mwenye matatizo ya akili aibe?”,alieleza Museven.
Katika hatua nyingine Museven kabla ya kumkata koromeo
mwanaye pia mwezi Julai mwaka jana Salvatory alitaka kumchinja mke wake Mariam
Idd lakini yeye (Museven) akawasuruhisha na mke wa mtuhumiwa kuamua kumkimbia
mme wake kwa hofu ya kuuawa na mwanamme kubaki na mtoto Said Joshua.
“Haikuishia hapo siku chache tu mtuhumiwa pia
alitaka kumchinja mtoto wa jirani yake kwa madai ya kwanini huwa anacheza na
mwanaye ,kama mwenyekiti wa kitongoji nikaingilia kati kitendo hicho kilimuudhi
Salvatory na kutaka kunichinja pia,nikaita polisi akakamatwa,na ndiyo tuhuma
iliyompeleka gerezani kwa kipindi cha miezi miwili,na mtoto kurudi kwa mama
yake”,alieeleza Museven.
Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo Mariamu Idd (35) alisema, mtoto wake alichukuliwa na baba yake mzazi siku moja kabla ya tukio na kwenda naye kwake mitaa ya Majengo kwa kuwa alikwisha achana na mwanamme huyo siku nyingi.
“Baba wa mtoto huyu siku za nyuma,alikuwa akimchukua mwanangu mara kwa mara na kumpeleka nyumbani kwake,mimi nilishaachana naye, huwa anamrudisha,na amekuwa akidai kuchoshwa na huduma za matibabu kutokana na mtoto huyo kuwa na matatizo ya kiafya”,alifafanua mama huyo.
0 Response to "MTOTO ALIYECHINJWA NA BABA YAKE NA KUTOKWA DAMU NYINGI SASA AFARIKI DUNIA"
Post a Comment