Na Kareny Masasy
Simiyu.
JESHI la polisi mkoani Simiyu limewataka wauzaji wa
tindikari mkoani humo kuhakikisha
wanasajiliwa na ofisi ya mkemia mkuu wa serikali, ili kutambulika kisheria
sambamba na kupewa utaratibu wa matumizi sahihi ya bidhaa hiyo kwa lengo la
kuondoa matumizi mabaya ya bidhaa hiyo ikiwemo kuwadhuru watu.
Mbali na hilo kamanda wa jeshi hilo Charles mkumbo amewatahadharisha
wananchi wote ,kuwa kwa yeyote atakayekutwa na tindikari mtaani, atakamatwa,
ikiwa pamoja na kufikishwa mahakani.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana kamanda
Mkumbo alisema kuwa katika utaraatibu uliowekwa kwa sasa kwa wauzaji wa bidhaa
hiyo unamtaka kila muuza tindikari kusajiliwa na ofisi ya mkemia mkuu,sambamba
na kupewa maelekezo ya jinsi ya kutumia au kuuza bidhaa hiyo.
Alisema kwa kila atakayehitaji tindikari kwa matumiuzi
sahihi, atatakiwa kuja na mtu au kupewa kibali na mtu atakayetumia tindikari
hiyo,kama kwenye magari au pikipiki atatakiwa kuja na fundi makenika dukani
kuchukua bidhaa hiyo.
Katika utaratibu huu
ambao ni mpya unao lenga kukomesha matukio ya kumwagiwa watu tindikari,utamtaka
muuzaji wa bidhaa hiyo kuhakikisha kila anayenunua tindikari anaitumia katika
matumizi sahihi na atakayeruhusiwa kutumia au kuja na
kibali”alisema.
Alibanisha kuwa baadhi ya maofisa kutoka ofisi ya
mkemia mkuu kanda ya ziwa iliyoko Jijini Mwanza wamewasili mkoani hapa na
watakuwepokwa siku kumi,ili kufanya usajili huo,sambamba na kutoa elimu pamoja
na utaratibu wa juu ya matumizi ya tindikari.
Kamanda huyo alieleza kuwa jeshi la polisi halitakuwa
na huruma kwa yeyote atakaye kutwa na tindikari mtaani, kuwa atakatwa na
kufikishwa katika vyombo vya sheria huku
akiwataka watumiaji wa bidhaa hiyo kufuata utaratibu huo mpya.
0 Response to "JESHI LA POLISI LAWATAKA WAUZAJI WA TINDIKARI KUJISAJIRI ILI WAPATIWE VIBALI"
Post a Comment