Na Kareny Masasy
Shinyanga.
WAZAZI na walezi wanaowasomesha watoto wao katika shule ya
msingi Bugoyi (A) iliyopo manispaa ya shinyanga wamekabidhi jumla
ya madawati sabini na mbili kwa ajili ya kuondokana na changamoto
ya kusoma na kuandika huku wakiwa wamekaa chini na kuwajengea
msingi wa kupata elimu bora.
Zoezi hilo
limefanyika jana wakati mwenyekiti wa kamati ya shule Peter Sangwa akikabidhi
madawati hayo kwa mkuu wa shule hiyo Suleimani Shabani Kipanya na kusema kuwa
lengo la kutengeneza madawati hayo limetimia kwa asilimia tisini ambapo walitarajia
kukabidhi madawati miamoja kutokana na baadhi ya wazazi kushindwa kukamilisha
michango yao kwa wakati.
kwa upande wake
mwalimu mkuu wa shule hiyo Suleimani Kipanya ameshukuru wazazi hao kwa
kujali maendeleo ya watoto wao katika suala zima la kuchangia miradi ya
maendeleo ya shule hiyo hali ambayo itawafanya wanafunzi hao kuongeza kiwango
cha kufauru kutokana na mazingira ya shule kuwa mazuri.
Kipanya amesema kuwa zaidi ya madarasa mawili ya
wanafunzi katika shule hiyo walikuwa wanasoma huku wamekaa chini zaidi ya
miaka miwili pia kwa kuanza na mwaka huu 2014 tatizo hilo limekwisha na
hakuna mwanafunzi anayesoma huku akiwa amekaa chini.
Amesema shule hiyo
mpaka hivi sasa itakuwa na jumla ya madawati 300 huku ikiwa na jumla ya
wanafunzi 1200 pamoja wanafunzi wa darasa la awali 126, walimu ishirini
na saba wakiume wawili,wakike ishirini na tano na ilianzishwa mwaka 1975.
Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa mbuyuni Chief
Abdalah Sube ambaye alishuhudia ukabidhiwaji wa madawati hayo amesema
kuwa jambo walilolifanya wazazi hao ni jema huku akiwataka wazazi wengine waige
mfano huo kwani kusomesha watoto katika mazingira mazuri ni kuwapatia urithi wa
elimu bora.
Sube amesema baadhi
ya wazazi katika shule za msingi
wamekuwa na tabia ya kuchanganya masuala
ya siasa na maendeleo ambapo suala likipelekwa hivyo linafanya
kushindwa kukamilisha michango ya madawati kwa ajiri ya watoto wao hivyo
kuwafanya wakiendelea kukaa chini pasipo na sababu za msingi.
0 Response to "WAZAZI NA WALEZI WAKABIDHIWA MADAWATI KWA PESA WALIZOKUWA WAMECHANGA."
Post a Comment