BAADHI ya wazazi wa kata ya Ndembezi
manispaa ya Shinyanga wamelalamikia uongozi wa shule ya msingi
Bugoyi (B) kwa kitendo cha kuchangisha shilingi 10,000
kwaajili ya madawati pindi wanafunzi walipokuwa
wakiandikishwa darasa la kwanza miaka mitatu mfululizo
iliyopita lakini matokeo yake mpaka sasa bado wakiendelea
kukaa chini.
Wakiongea na mwandishi wa habari
aliyetembelea katika kata hiyo walisema kuwa walimu walitilia mkazo
wa utozwaji wa shilingi 10,000 kwaajili ya mchango wa madawati huku
wakidai kuwa kama fedha hizo hazitatolewa mwanafunzi hataandikishwa
shule.
Wazazi hao walisema kuwa kiasi cha fedha walichokuwa
wakitozwa kwa kutishiwa watoto wao kutoandikishwa shule mpaka wawe
wamekitoa, wamesikitishwa kwa kuoana bado wanaendelea kukaa chini
huku fedha hizo wakiwa tayari wamekwisha lipia tangu kuanza kwao darasa la
kwanza.
Mmoja wa wazazi hao Jenipher Subi alisema
kuwa mtoto wake aliandikishwa darasa la kwanza mwaka 2012 akitoa
michango yote iliyokuwa ikihitajika shuleni hapo ikiwemo dawati
chakushangaza mwaka huu yuko darasa la tatu bado anaendelea kukaa
chini huku akiutaka uongozi wa shule kutoa ufafanuzi wa kina ili
kufahamu nini tatizo.
“Kweli inasikitishwa kwa kuona watoto wakiendelea kukaa
chini wakati wazazi tumelipa, walipokuwa wakiandikishwa darasa la kwanza
waliweka msisitizo mtoto hawezi kuandikishwa mpaka awe amelipa mchangao
wa dawati kiasi cha shilingi 10,000 ambapo tulitegemea wanafuzni
watakuwa wakisoma wakiwa wamekaa kwenye madawati hali ambayo imekuwa kinyume
sasa tatizo lipo wapi”alisema mzazi huyo.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Anord Rweshabura
alisema kuwa shule hiyo inajumla ya wanafunzi zaidi ya 900 waliochangia
madawati hawafiki 30 ikiwa michango iliyotolewa na wazazi imepelekwa kukarabati
madawati yaliyokuwepo ambapo wanaokalia madawati hayo ni darasa la
kwanza, darasa la pili na darasa la saba madarasa yaliyobaki wanakaa
chini.
Naye mratibu wa elimu kata ya Ndembezi Bulugu Selemani
alisema kuwa changamoto kubwa iliyopo baadhi ya wazazi wamekuwa hawatoi
michango hiyo kama wanavyokubaliana kwenye vikao,utakuta waliochanga
hawafiki zaidi ya 50 ikiwa dawati moja linauzwa shilingi 70,000
mpaka shilingi 80,000 na fedha hizo hazitolewi kwa wakati ndio
tatizo wanafunzi kuendelea kukaa chini.
Diwani wa kata ya hiyo David Nkulila ambaye pia ni naibu
meya wa manispaa ya Shinyanga alisema kuwa malalamiko ya baadhi ya wazazi
yamemfikia kuhusiana na tatizo hilo ikiwa tayari ameweka mikakati ya kuitisha
mkutano wa hadhara ili kuweza kukutana kwa pande zote kwa mwenye hoja na
kujibiwa lengo kuweza kupata ufumbuzi wa nini kifanyike.
0 Response to "BAADHI YA WAZAZI KATA YA NDEMBEZI WALALAMIKIA UONGOZI WA SHULE"
Post a Comment