MKOA wa Shinyanga umefanikiwa kuingiza kidato cha kwanza
wanafunzi wote waliomaliza elimu ya msingi na kufaulu kwa mwaka jana.
Katika taarifa iliyotolewa
kwa waandishi w a habari jana kaimu afisa elimu wa mkoa wa Shinyanga
ambaye ni afisa elimu ya watu wazima
mkoa huo Yohana Mkumbo amesema kuwa zaidi
ya wanafunzi 28,000 kati yao wanafunzi 13604 walifaulu mtihani huo kujiunga
na kidato cha kwanza .
Mkumbo amefafanua kuwa kati ya wanafunzi hao wavulana ni 7460 na
wasichana ni 6144 na kuongeza kuwa wilaya ya Kahama inaongoza kwa kufaulisha
wanafunzi 3868 ikifiatiwa na wilaya ya halmashauri ya mji wa Kahama
iliyofaulisha wanafunzi 2953.
Amesema katika idadi
hiyo manispaa ya Shinyanga imefaulisha wanafunzi 2297, wilaya ya Kishapu wanafunzi
2266 huku wilaya ya Shinyanga ikifaulisha wanafunzi 2220 ambapo mkoa
umefanikiwa kuwaingiza kidato cha kwanza wanafunzi wote waliofauli kwa asilimia
100.
Aidha amesema kuwa
licha ya mkoa kujivunia hatua hiyo lakini bado unakabiliwa na changamoto ya
mwitikio mdogo wa elimu kwa upande wa wazazi hali inayopelekea baadhi ya
wanafunzi kukatisha masomo ambapo jumla ya wanafunzi 458 hawakufanya mtihani
huo kutokana na sababu mbalimbali.
Kwa upande wa changamoto ya uhaba wa maabara kwenye baadhi ya shule amesema kuwa mkoa unafanya jitihada za makusudi ili
ifikapo mwaka 2015 mkoa uwe umetatua
tatizo hilo kwa shule zote za sekondari ambapo ikiwa mkoa una maabara 59 huku mahitaji halisi
ni maabara 347.
0 Response to "WANAFUNZI WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA WAPATA NAFASI WOTE"
Post a Comment