MADIWANI wa halmashauri
ya manispaa ya Shinyanga wametaka kuondolewa katika
orodha ya kuchangia fedha kituo maalumu cha kulelea
watoto wenye ulemavu mbalimbali Buhangija ikiwa katika
mchango huo manispaa imelezwa kuchangia kiasi cha shilingi millioni 24.
Hatua ya kukataa
kuchangia imetokana na kituo hicho kulea watoto wanao
toka maeneo tofauti kama vile mkoa wa Geita,Simiyu, Tabora, Mwanza
pamoja na Shinyanga hali ambayo mikoa hiyo imekuwa haitoi msaada
wowote.
Madiwani hao
wakiongea katika baraza la madiwani jana
lililofanyika kwenye ukumbi wa mkoa wamesema kuwa hawatakuwa tayari kuchangia pesa hizo
kutokana na kituo hicho kuwa ndani ya manispaa na majukumu mengi
wamekuwa wakikabiliana nayo,
Naibu mstahiki
meya David Nkulila amesema kuwa hali ya kituo hicho
hairidhishi kutokana na kuachanizwa kwa manispaa pekee kutunza watoto
hao isitoshe imepangiwa kuchangia shilingi millioni 24 ambapo
haiwezekani
Mkuu wa kituo hicho mwalimu Peter Ajali
amesema kuwa watoto walipo ni
258 ambapo walemavu wa ngozi 172,wasioona 48,viziwi 38 ikiwa changamoto kubwa iliyopo ni
uhaba wa chakula na deni la shilingi millioni 4.8 kutoka mamlaka ya
maji manispaa (Shuwasa) kudai kituo hicho.
Ambapo suala la deni la
maji injinia kutoka shuwasa Slyvesta Malole alieleza madiwani kuwa deni
hilo linadaiwa tangu mwaka jana huku akilalamika kutofahamu hali
halisi ya maisha ya kituo hicho kwa watoto ikiwa alisisitiza kuwa akaunti
inayosoma kwa sasa ibadilishwe na kufahamika na deni hilo lazima lilipwe.
Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Annarose Nyamubi alisema kuwa kwa upande wa wilaya ya
Bukombe mkoa wa Geita kuna watoto zaidi ya 30 hivyo idara ya maendeleo ya
jamii wanatakiwa kufanya mawasiliano ili halmashauri ziwatambue watoto wao pia
suala la kuletwa watoto wapya kila siku waletwe kwa utaratibu utakao
ridhia pande zote mbili.
MWISHO.
0 Response to "MADIWANI WAKATAA UTOAJI WA SHILINGI MILLIONI 24 KWENYE KITUO CHA KULELEA WATOTO WENYE ULEMAVU"
Post a Comment