Habari za hivi Punde

WAGONJWA MKOANI SHINYANGA WALALAMIKIA HOSPITALI YA MKOA KUKOSA DAWA MARA KWA MARA



Na  Kareny  Masasy
Shinyanga.

 WAGONJWA wenye malaradhi mbalimbali wakiemo wa malaria mkoani Shinyanga  mara nyingi wamekuwa wakikumbwa na uhaba wa dawa  pamoja na vifaa tiba ndani ya hospitali hiyo ambapo hulazimika kwenda kununua katika maduka ya dawa  ya watu binafsi .

Wakiongea na  mwandishi wa habari hospitali aliyetembelea hospitalini hapo  baadhi ya wagonjwa walisema kuwa dawa katika hospitali hiyo zimekuwa zikija kwa msimu  wakati mwingine unakuta dawa zipo ambapo muda mwingine tena ukirudi unaelezwa dawa hakuna.

 Walisema hospitali ya mkoa imekuwa na changamoto ya ukosefu wa dawa mara kwa mara inafikia hatua ya mpaka kubahatisha , kwani zimekuwa  upatikanaji wake wa  msimu wakati  mwingine zinakuwepo na sio dawa  za aina zote isitoshe hata vifaa tiba  kwa wagonjwa wanaofanyiwa  oparesheni  ndogo inabidi vikanunuliwe na mhusika.

Mmoja wa  wagonjwa waliohudhuria hospitalini hapo  Dotto Juma alisema kuwa dawa  kwa sasa zinapatikana sio za aina zote  bali zingine hulazimika kwenda kununua katika maduka ya watu binafsi kama vile vidonge vya watu wenye vifua vya kubana (Athumar)  jambo ambalo linaonyesha  hospitali hiyo kutokuwahuduma zilizojitosheleza.

“Dawa zimekuwa za msimu kuna wakati unapatiwa dawa za aina zote ulizoandikiwa na daktari  lakini kuna wakati hakuna hata  aina moja ya dawa inayopatikana, angalau  kwa wale wanaoumwa malaria  kwao inakuwa  nafuu,magonjwa mengine ikiwemo kubanwa kifua (athumar)   dawa zake zimekuwa adimu  mpaka uende kununua maduka ya watu binafsi  tena kwa gharama kubwa”.

Kwa upande wake  mganga mfawithi wa hospital hiyo Dkt    Fredrik Mlekwa  wakati akiongea na mwandishi wa habari  baada ya kupata malalamiko  ya wagonjwa kukosa dawa ikiwemo vifaa tiba alisema  huchelewa kuwafikia  hali ambayo imepelekewa wagonjwa   kupata changamoto ya ukosefu wa dawa hospitalini hapo.

Hata hivyo Dkt Mlekwa  alisema kuwa  katika suala hilo aliiomba Serikali  kuangalia upya utaratibu wake wa kusambaza madawa pamoja na vifaa tiba viweze kufika kwa muda muafaka,huk akilalamikia kitengo cha  bohari ya dawa  (MSD) kilichopewa jukumu la kusambaza  wamekuwa wakichelewa kufikisha na pia kuleta  vifaa  ambavyo hawaku agizwa..
  “Bohari ya dawa (MSD) ambayo wamekuwa wasambazaji wakuu    uwezo wao wakusambaza dawa ni asilimia 25 au 30 na asilimia inayobaki   hununua dawa kidogo kwa vyanzo vilivyopo hospitalini hapo  ambazo hazitoshelezi mahitaji ya idadi ya wagonjwa wa kila siku wanaohudhuria hospitalini”alisema  Dkt Mlekwa.
MWISHO.

0 Response to "WAGONJWA MKOANI SHINYANGA WALALAMIKIA HOSPITALI YA MKOA KUKOSA DAWA MARA KWA MARA"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.