)ASKARI
watatu wa jeshi la Polisi wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Ruvuma (Homso) iliyopo mjini songea Mkoani humo wakiwa wanapatiwa
matibabu ya majeraha ambayo waliyapata baada ya kushambuliwa kwa kitu
kinachodhaniwa kuwa ni Bomu la kurushwa kwa mkono.
Tukio
hilo limetokea September 16/ 2014 majira ya saa moja na nusu usiku
katika kata ya Msufini karibu na daraja la Matarawe, wilayani Songea
Mkoani Ruvuma ambapo watu watatu wasio fahamika walitupa kitu kinacho
sadikiwa kuwa ni Bomu la kutupwa kwa mkono ambalo limetengenezwa
kienyeji na kuwajeruhi askari hao watatu waliokuwa doria.
Askari
hao waliojeruhiwa ni WP. 10399 PC Felista aliyejeruhiwa mguu wa kulia
kwenye unyayo na pajani ,G. 7351 PC Ramadhani aliye jeruhiwa mguu wa
kulia karibu na goti na tumboni upande wa kulia na G. 5515 pc John
aliyepata majeraha katika mguu wa kulia chini ya goti na jeraha dogo
tumboni.
Mganga
mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr. Daniel Malekela ameeleza kutoa
vipande vya bati na misumari katika majeraha ya askari hao na mpaka sasa
wanaendelea na matibabu.
Alisema
kufutia hali hiyo Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linaendelea na
uchunguzi wa kina ili kuwakamata wahusika wa tukio hilo kwa hatua zaidi
za kisheria.
Kwa
upande wake Mkuu wa mkoa wa Ruvuma SAID MWAMBUNGU amesikitishwa na
kitendo hicho cha wahalifu kujeruhi askari tena kwa makusdi na amesema
serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha
wanawasaka na kuwakamata.
Eneo la tukio ambalo kitu kinachosadikiwa likiwa limezungushiwa alama na Jeshi la Polisi.
Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwangu akizungumza jambo na waandishi wa habari
katika hoptal ya mkoa wa Ruvuma baada ya kuwatembelea majeruhi hao.
Kamati ya ulinzi na Usalama wakiwa Hospital ya mkoa wa Ruvuma.
Aliyelala kitandani ni WP ambaye amejeruhiwa akiwa amelazwa katika hospital ya Mkoa wa Ruvuma.
Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr Daniel Malekela akizungumza na wandishi wa habari hopitalini hapo.
0 Response to "ASKARI WASHAMBULIWA KWA MABOMU WAJERUHIWA VIBAYA-KYELA MBEYA."
Post a Comment