Wito umetolewa na
chama cha msalaba mwekundu mkoani Shinyanga kwa wananchi kujitokeza kuchangia damu salama ambapo
mazoea yaliyojengeka ni pale
wanapopatwa na mgonjwa nayehitaji damu ndipo huchukua jukumu la kujitokeza kuchangia damu hiyo bila kuwa na hofu yoyote.
Hayo yalisemwa na mratibu wa damu salama wa chama hicho mkoa Anna Lusana
wakati alipokuwa akiongea na mwandishi wa BLOG HII ofisini
kwake,huku akieleza kuwa kwa mwaka jana waliweza kupata jumla ya uniti 4145 za damu salama sawa na asilimia 80 ikiwa lengo ni
kufikia uniti 5000.
Lusana alisema kuwa
jamii inauelewa juu ya kuchangia
damu ila bado wana hofu kubwa ya kupimwa maambukizi ya virusi sanjari na imani potofu waliyonayo kwa baadhi, ambapo uchangiaji wa damu mara nyingi wamekuwa wakijitokeza pale
wanapokuwa na mgonjwa anayehitaji kuongezwa damu salama,pia changamoto
nyingine kutegemea hasa wanafunzi mashuleni.
“Imani potofu iliyopo
kwa baadhi ya wananchi hasa maeneo ya vijijini
kuwa wakitoa damu wataugua,hofu ya kupimwa maambukizi ya virusi ikiwa
pia hutegemea zaidi wanafunzi wa shule ya sekondari waliofikisha umri wa miaka 18 nao ni wachache
ikiwa wengi wao hawajafikisha umri huo, na mazoea yaliyopo mtu kutoka damu
mpaka awe na mgonjwa mwenye mahitaji ya
kuongezwa damu salama na kujitokeza hiyo ndio changamoto” alisema Lusana.
Lusana alisema kuwa upatikanaji wa damu salama mara nyingi
wamekuwa na vigezo kwa kuangalia historia ya maradhi ya mtu anayetaka kujitolea damu asiwe
ametibiwa muda wa miezi mitatu na kuna
makundi ambayo ni wale wanaojitolea kwa
hiari, wenye wagonjwa wa mahitaji ya kuongezwa damu salama, pamoja na kwenye mikusanyiko ya watu kama minadani ambayo upatikanaji wake asilimia kubwa damu yake siyo salama kwenye kundi hilo.
|
0 Response to "UPATIKANAJI WA DAMU SALAMA MKOANI SHINYANGA BADO KUNACHANGAMOTO"
Post a Comment