Habari za hivi Punde

KAIMU AFISA KILIMO,UMWAGILIAJI NA USHIRIKA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI AKIWA KATIKA ZIARA YA UKAGUZI WA MASHAMBA YA MAZAO MBALIMBALI.

Hili ni moja la zao la ufuta katika shamba darasa lililolimwa na mbwana Shayo katika kijiji cha Kwakonje wilayani Handeni.

Kaimu afisa kilimo ,umwagiliaji na ushirika  Yibarila Chiza Kamele akiwa na meneja masoko wa   pembejeo Hamza  Ibrahim wakikagua shamba  lenye zao la ufuta 

Kaimu afisa kilimo ,umwagiliaji  na ushirika  akiwa katika moja la shamba lililolimwa kwa kufuata kanuni za kilimo bora  

Baadhi ya  wakulima wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na mtaalamu Hamza Ibrahim na kuwasihi kutumia mbolea kwa wakati wa kuanza kupanda na baada ya kuchipua  huku akieleza kuwa  shina moja lenye  magunzi mawili ya mahindi yaliyojaa vizuri huweza kutoa robo kilo ya  mahindi,ambapo pia wameelezwa kutokubali kupima mahindi yao kwa gunia pindi wanapouza bali wapime kwa kilo ili waweze kupata faida .

Hapa meneja wa masoko ya pembejeo Hamza Ibrahimu akimuonyesha  a kaimu afisa kilimo mbegu mpya itakayo anza kutumika kwa msimu wa kilimo wa mwaka  huu.


0 Response to "KAIMU AFISA KILIMO,UMWAGILIAJI NA USHIRIKA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI AKIWA KATIKA ZIARA YA UKAGUZI WA MASHAMBA YA MAZAO MBALIMBALI."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.