Habari za hivi Punde

HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI WAKULIMA WAKE WAKUMBWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI KATIKA UZALISHAJI MAZAO NA UVUNAJI IKIWEMO MASOKO.

Kaimu afisa kilimo,umwagiliaji na  ushirika  Yibarila  Chiza akiwaelezea waandishi wa habari ambao hawapo pichani mazao mbalimbali yanayolimwa katika wilaya ya Handeni na changamoto ya ukosefu wa masoko  huku akisikitishwa na baadhi ya wakulima kuendelea kutumia zana ya jembe la mkono na kutofuata kilimo cha utaalamu.

Kaimu afisa kilimo ,umwagiliaji na ushirika Yibarila Chiza  Kamele akiangalia shamba darasa la zao la mtama katika kijiji cha Mazingara kata ya Mkata wilayani Handeni mkoani Tanga.

Chandaru chatumika katika matumzi yasiyo sahihi kwa malengo yake ikiwa vijana hawa walikutwa wakitumia chandarua hicho kuchekecha  zao la ufuta jambo ambalo liliwashangaza waliokuwa wametembelea kijiji  cha Mazingara kata ya mkata  ambapo wanaishi ndani ya kitongoji cha  Mbuzi.

Mwenyekiti  wa kijiji cha Kwachaga Tuliani  katika halmashauri ya wilaya ya  Handeni  Miraji  Ahamed akiwa katika trekta ya kijiji hicho ambalo ndio mradi wa kuongeza kipato ambao  ulimwaji wa ekari moja hukodishwa kwa shilingi 40,000.

0 Response to "HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI WAKULIMA WAKE WAKUMBWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI KATIKA UZALISHAJI MAZAO NA UVUNAJI IKIWEMO MASOKO."

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.