Habari za hivi Punde

MKUTANO WA UWT SHINYANGA VIJIJINI WAFANYIKA,WATU WENYE ULEMAVU WAPEWA MSAADA WA BAISKELI

Ni katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambako leo kumefanyika mkutano wa UWT wilaya ya Shinyanga vijijini kujadili mambo mbalimbali kuhusiana na wanawake kuwa mstari wa mbele kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zinazokuja za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2015

Aliyeshikilia kipaza sauti(mic) ni mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga bi Helena Daudi akitambalisha wageni walioko meza kuu akiwemo katibu wa ccm mkoa wa Shinyanga Adam Ngalawa(kulia kwake)

Wajumbe wa UWT kutoka kata 26 za wilaya ya Shinyanga vijijini wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika mkutano huo,ambapo ajenda mbalimbali zilitolewa na viongozi wakiwemo wabunge wa viti maalum ambao ni Mheshimiwa Azza Hilal na mheshimiwa Lucy Mayenga ambaye ni mkuu wa wilaya ya Uyui mkoani Tabora


Mbunge viti maalum Lucy Mayenga akizungumza wakati wa mkutano wa UWT ambapo aliwataka wanawake kuwa wabunifu,wajasiriamali ili kujinyanyua kiuchumi katika familia zao.Pia aliwasisitiza kujenga tabia ya kuhifadhi fedha badala ya kuzitumia kwenye mambo yasiyofaa kwani hali hiyo inachangia kuwepo kwa umasikini katika jamii.

Mbunge wa viti maalum ccm mkoa wa Shinyanga Azzah Hilal akizungumza kuhusu mchakato wa katiba mpya ambapo alisema mchakato wa katiba ni siasa hivyo wananchi wasidanganyike kwamba kuwa na serikali tatu kutaondoa kero za wananchi kwani zitaongeza gharama hivyo suluhisho la kero za watazania ni serikali mbili pekee,ambazo zitaendelea kuifanya nchi kuwa kisiwa cha amani

Mbunge wa viti maalum Azzah Hilal akiendelea kuzungumza na wajumbe wa UWT wilaya ya Shinyanga vijijini leo mjini Shinyanga

Baadhi ya wajumbe wa UWT wilaya ya Shinyanga vijijini

Hizi ni baiskeli 8 kwa ajili ya watu wenye ulemavu zilizotolewa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azzah Hilal baada ya mkutano wa UWT wilaya ya Shinyanga vijijini kumalizika leo mjini Shinyanga.  




Mbunge wa viti maalum ccm mkoa wa Shinyanga Azzah Hilal akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli kwa ajili ya watu wenye ulemavu.Mbele wa kwanza kulia ni bi Anna Sengati kutoka Kata ya Tinde,kushoto kwake ni bi Nyanzobe Jimwenda kutoka kata ya Nyamalogo,wa tatu ni Zainabu Juma  kutoka kata ya Itwangi ambao ni miongoni mwa watu wenye ulemavu waliozaliwa nao waliopata msaada wa baiskeli kutoka kwa mbunge leo
Watu wenye ulemavu wakiwa kwenye baiskeli walizopewa na mbunge Azzah Hilal leo mjini Shinyanga

Mtoto mwenye ulemavu akiwa amekaa kwenye kiti cha magurudumu,ambacho ni miongoni mwa viti vilivyotolewa na mbunge huyo wa ccm shinyanga

Mbunge wa viti maalum ccm mkoa wa Shinyanga Azza Hilal akishikana mkono wa shukrani na bi Nyanzobe Jimwenda,ambaye ni mlemavu ambaye alimshukuru mbunge huyo kwa msaada wa baiskeli kwani itamsaidia katika shughuli zake mbalimbali za kujitafutia kipato

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga akiwa amembeba mtoto mwenye ulemavu Medard Hamis mwenye umri wa miaka mitatu.Mbunge huyo alisema ameguswa kwa kiasi kikubwa na watu wenye ulemavu na kwamba anatambua wako wengi wenye mahitaji lakini amewafikia wachache (watu wanane)na kuongeza kwa jukumu la kuwatunza na kuwalea walemavu la watu wote katika jamii na kwamba watu wenye ulemavu hawakupenda kuwa hivyo.

0 Response to "MKUTANO WA UWT SHINYANGA VIJIJINI WAFANYIKA,WATU WENYE ULEMAVU WAPEWA MSAADA WA BAISKELI"

Post a Comment

KARENY. Powered by Blogger.